Ndugu zangu waandishi wa habari
Habari za kazi, na hongereni sana kwa kazi nzuri ya habari mnayoifanya
katika jamii yetu.
Ndugu zangu nimewaiteni hapa ili kusema machache na
kuendelea kutoa maoni yangu binafsi kama mwanachama hai wa Umoja wa vijana (Uvccm)
kuhusu kumsisitiza mzee John Samwel Malecela auombe radhi Umoja wa vijana
waTanzania kwa kitendo chake cha kuunga mkono tamko lilitolewa na mkuu wa idara
ya uhamasishaji na chipukizi wa uvccm Tanzania Ndg Paul Makonda,,
Msisitizo wangu unatokana na jinsi gani nilivyosikitishwa na
kitendo alichokifanya Mzee Malekela cha kumuunga mkono ndg Makonda,, ambae
tamko lake limekataliwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa ndg Sadifa Juma Khamis, kwamba si la umoja wa
vijana na si vema kwa wanachama kusemana nje ya vikao, pia makamu mwenyekiti wa
Umoja wa Vijana wa Tanzania Ndg Mboni Muhita pia amelikataa ya kwamba
halitokani na Umoja wa vijana, ikumbukwe kwamba Makamu Mwenyekiti ni mtu wa
pili kiitifaki katika umoja wa vijana ukilinganisha na Ndg makonda ambae ni watano
katika uvccm. Na ni kiongozi wa idara tu. Mzee malekela kuliunga tamko la
Makonda ni kinyume cha utaratibu na amewakosea heshima viongoz wetu wa vijana
wa taifa na uvccm yote kwa ujumla.
Mbali na hilo,
pia tamko la ndg Makonda limebeba misamiati tata ambayo imesababisha mgongano
wa hoja baina ya viongoz wa kiimani na waumini wao wa madhehebu yote ambayo pia
ni sehemu ya taifa hili.. mgongano huo wa viongoz wa kiimani na Chama unaweza
ukakiathiri Chama chetu kwa kiasi kikubwa.
Ni rahisi sana kwa viongozi wa kiimani kumsamehe ndg Makonda
kutoka na rika lake, lakini ni vigumu sana kumuelewa Mzee wa chama kwa kuunga
mkono na wanaweza wakahisi kwamba chama kimemtuma ndg Makonda kwenda
kuwahusisha katika tamko lake, jambo ambalo sio la kweli. Lkn pia nasikitishwa sana kumuona Mzee wetu huyu kuunga mkono tamko
linalomdhalilisha mkt wetu wa vijana taifa na watendaji wake kwa mtu mmoja
kuivunja kanuni mbele yao,
huku akiudanganya umma kwamba ni tamko la Uvccm..
Ndugu zangu waandishi, naendelea kusisitiza kwamba Mzee
Malecela auombe radhi umoja wa vijana Tanzania..
Pamoja na hayo,, pia napenda kutoa maoni yangu binafsi
kuhusu maelezo ya mkt wa uvccm mkoa wa Morogoro aliyoyatoa jana kwa waandishi
wa habari, yale yalikuwa ni mawazo yake binafsi na sio ya umoja wa vijana
kwakuwa hayajapitia katika kikao cha kamati ya utekelezaji cha mkoa,, amefanya
vema kuujulisha umma kwamba maoni niliyoyatoa mimi awali yalikuwa ni maoni
yangu binafsi na si ya uvccm mkoa kama nayeye pia maoni aliyoyatoa ni yake
binafsi na si ya uvccm mkoa waMorogoro.
Na chama kinaruhusu mtu kutoa maoni yake binafsi, nampongeza sana
Lakini pia, si jambo jema kwa kila anayetoa maoni binafsi
kuhusu mustakabali wa chama, kuyahusisha maoni yake na maswala ya makundi,, na
chama chetu hakijamzuia mwanachama yeyote mmoja mmoja kutoa maoni yake
binafsi,, tukianza kuwanyima fursa wanachama kutoa maoni yao kwa mihemko ya
makundi, basi tutaikandamiza demokrasia ya ndani ya chama, kama viongoz ni
lazima tujue kutofautisha kati ya vichwa vya habari vya habari na habari
yenyewe, vinginevyo kutokana na ukubwa wa chama na maoni yanayotolewa na
wanachama wa maeneo mbalimbali ya ndani na nje
ya nchi, kutakuwa na watu wa kukanusha au kurekebisha, na wale wa kutoa
maoni, CCM ni chama cha wanachama wote,, pasiwepo namna yeyote ile ya kunyimana
uhuru.
Naungana na Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Morogoro kumpongeza
sana mkt wetu mpendwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Jakaya
Mrisho Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa mkoani Mbea hivi karibuni katika
sherehe za kutimiza miaka 37 ya chama chetu imara cha CCM, ni wajibu wetu sote
kuyatekeleza yale aliyotuagiza mhe mkt wetu wa CCM taifa. Na hasa kuheshimu
maamuzi yatokanayo na vikao
Ndg zangu mkoa wa Morogoro umekumbwa na matatizo mengi sana,
ikiwa pamoja na mapigano ya wakulima na wafugaji, na mafuriko yaliyotokea
wilayani kilosa na mvomero,, nami napenda kutoa pole kwa wahanga wa matatizo
hayo, na kuunga mkono maoni ya mkt wa uvccm mkoa kwa wadau mabalimbali
kujitokeza katika kusaidia wahanga, pia nawapongeza sana viongozi wa serikali
na chama wote kwa kuwajibika kutatua na kusaidia katika swala hili..
Lakini ni vema sana kwa sisi vijana kuwa wa kwanza na mstari
wa mbele kufika katika maeneo ya matukio mapema ili kuona hali na kushiriki
katika hatua za awali,, tusijifunze kutoa pole kwenye vyombo vya habari baada
ya matukio kuwa yameshapita na hatujafika hata eneo lenyewe la tukio.. hapo
tutakuwa tunaonekana tunafanya siasa badala ya kazi.. lakini kutoa maelekezo au
wito katika maeneo ya majanga ambayo tayari mkt wetu wa taifa ameshafika na
kufanya hivyo, ni makosa ambayo tunahitajika kujifunza…
Napenda sana kutoa pongez zangu binafsi kwa vijana wa uvccm
wilaya ya mjini na wale wa kilosa kwa jinsi wanavyoshiriki kikamilifu katika
shughuli za kampeni katika katika chaguz za marudio kata ya tungi na ludewa, ni
maoni yangu binafsi kwamba na sisi wanachama wengine tushiriki kikamilifu,
badala ya kutoa maoni huku tukiwa hatujawahi hata kufika katika eneo la tukio.
Hasa katika maeneo amabayo kuna chaguzi za marudio ndani ya taifa letu
Pia ni maoni yangu kwa vyama siasa hususani chadema kuacha
kampeni za vurugu na kujeruhiana ambazo zinawadhuru wananchi, kuwanyima amani
na kuzorotesha shughuli zao za kiuchumi, tufanye kempeni za kiistarabu, za hoja
na amani kama ilivyo desturi ya nchi yetu, pia
vyombo vya ulinzi naviomba viongeze umakini zadi katika kipindi hiki hasa
katika maeneo yale ambayo kampeni zinafanyika..
Asanteni kwa kunisikiliza, nawatakia kazi njema!!
IMETOLEWA NA
HERI HOZA
Mjumbe wa kamati yautekelezaji ya baraza la UVCCM
Mkoa wa Morogoro
0 comments:
Post a Comment