Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akitia saini mkataba ukarabati wa barabara za Mlapako, Kingo, Kitope na Nguzo katika manispaa hiyo
Meya huyo akitia saini mikataba hiyo katika eneo la Barabara ya kitope maarufu kama Shani sinema.
Meya Nondo akitia saini mkataba wa barabara ya Kingo kata ya Sabasaba katika manispaa ya Morogoro
Hapo utiliaji wa saini ukiendelea.
Meya huyo akikabidhi mkataba kwa mkandarasi wa kampuni ya C.G.I ya Morogoro.
Jamani mkafanya kazi vizuri kwa uaminifu, ni maneno ya meya wakati akikabidhi mkataba wa ukuarabati wa barabara hizo kwa mkandarasi wa kampuni ya barabara ya Victoria.
Meya huyo akikata utepe katika barabara ya Kitope kama ishara ya kuzindua ujezni huo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma akishuhudia uzinduzi huo katika eneo la barabara ya Kitope
meya huyo akiwa na viongozi wa manispaa katika eneo la Uruguru
Hali ilivyo sasa katika barabra ya Kitope ambayo itaanza kukarabatiwa hivi karibuni
Meya huyo akielezea jinsi mikataba hiyo inavyotakiwa kuanza na kumalizika kwa wakati
HALMASHAURI ya manispaa ya Morogoro imetia saini mkataba wa
ujenzi wa barabara tano zenye urefu wa kilomita 1.48 kwa kiwango cha rami kwa
gharama ya shilingi bilioni 1,148,932,800
na kampuni ya C.G.I ya mkoani hapa.
Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo alisaini mkataba
huo jana katika eneo la barabara ya Kitope na kuukabidhi kwa kampuni hiyo
kwaajili ya kuanza ujenzi huo.
Meya huyo alisema kuwa ujenzi huo unatarajiwa kuanza Februari
27 mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Julai 18 mwaka huu.
Aidha alisema kuwa barabara zitakazohusika na ujenzi huo wa
kiwango cha rami ni pamoja na Barabara ya Mlapakolo, Kingo , Kitope hadi posta ,
Nguzo hadi barabara ya Boma , Morogoro sekondari shule ua msingi Bungo.
Pia manispaa hiyo imetiliana saini na kampuni zingine tatu
kwaajili ya ujenzi wa barabara katika kata ya Boma, Tungi Mji Mkuu kwa kiwango cha Changarawe.
Alisema kuwa kampuni hizo ni SHilo Construction Co. Ltd ya
mjini hapa ambayo itajenga barabara ya Uruguru kilomita 0.733 kwa kiwango cha
changarawe kwa gharama ya shilingi 71,299,500 na ujenzi wake utaanza februari
27 na kumalizika Mei 19 mwaka huu.
Alitaja kampuni nyingine kuwa ni Victoria Earth Plan ya
mjini hapa ambayo itakarabati barabara ya Rwegasore kilomita 1.063 kwa kiwango
cha Changarawe. Kwa gharama ya shilingi
milioni 159,321,150 ambapo ujeniz
wake unatarajia kuanza Februari 27 mwaka huu na kumalizika Mei 19 mwaka huu .
Meya huyo aliwataka wananchi katika manispaa hiyo kutoa
ushirikiano kwa wakandarasi hao ili kuepuka vitendo vya kuhujumu vinavyoweza
kufanywa na baadhi ya wanancho wasio waaminifu.
Kwa upande wake injinia wa manispaa ya Morogoro Abdul Digaga alisema kuwa katika ujenzi wa barabara
hizo watafanya zoezi la bomoa bomoa kwa wamiliki wa nyumba waliojenga ndani ya
barabara ili kupisha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.
Kwa upande wake madiwani wa kata ya Mjini mkuu Hasan Maringo
alisema utiliaji saini mikataba hiyo ni utekelezaji wa ahadi ambazo madiwani
hao waliahidi kwa wananchi na kwamba ni
moja ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment