Mwenyekiti wa jumuiya ya serikali za Mitaa ALAT Taifa Didas Masaburi kulia, meya wa manispaa ya Morogoro ambaye pia ni mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Morogoro Amir Juma Nondo katikati na katibu wa ALAT Habraham Shamumoyo wakati wa kikao cha wadau wa ALAT kilichofanyika mjini Morogoro.
Wadau wa ALAT wakiwa na viongozi wao wakuu katika picha ya pamoja
Wajumbe wa ALAT wakifutilia mkutano huo kwa makini.
Ipo haja ya kususia uchaguzi wa serikali za mitaa kama katiba mpya haitatutamka ipasavyo, ni maneno ya Daniel Okoka makamo mwenyekiti wa ALAT Taifa.
Habari zaidi soma hapo chini.
MWENYEKITI
wa jumuiya ya serikali za Mitaa Taifa ALAT Didas Masaburi amesema kuwa wameazimia kwenda Dododma
kuwaomba wabunge wakatae kukaa vikao vya kujadili rasimu ya pili ya katiba mpya na kwamba irudishwe kwa wananchi ili iwekwe
vipengele vinavyozingatia masuala ya serikali za mitaa.
Masaburi
alisema hayo Februari 17 mwaka huu wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa wadau wa ALAT
uliofanyika mjini Morogoro.
Alisema kuwa
katika rasimu hiyo serikali za mitaa
imetamkwa kuwa itashiriki kama nchi
washiriki na kwamba haikuipa umuhimu wake.
Alisema kuwa
ili wananchi wengi waweze kushiriki kikamilifu hakuna njia inayoweza kuwakutanisha
isipokuwa ni serikali za mitaa.
‘’ Hakuna
baraza linaloweza kuwashirikisha wananchi wakashiriki kikamilifu bali ni njia
ya serikali za mitaa, lakini katika hii mpya haijaitamka ipasavyo na kwamba
tunaona serikali za mitaa zimeonekana hazina umuhimu, maendeleo mengi
yanafanywa kupitia serikali za mitaa sasa leo kama haijashirikishwa kikamilifu
sio ndio inakosa maana’’ Alisema
Alipongeza
Rais Jakaya Kikwete kwa kuhakikisha miundombinu ya kitaifa imeimarika ipasavyo
na kuongeza kuwa ili nchi iweze kutanuka zaidi hakuna budi kupanua miundombinu
ya ndani ambayo inatokana na serikali za mitaa.
Alisema kuwa
katiba hiyo ilijadiliwa kwa mfumo serikali mbili kwa maana ya Zanzibar na
Tanzania na kwamba kama muundo wa Nchi tatu Watanganyika hawajashiriki hivyo
katiba hiyo irejeshwe na kujadiliwa na Watanganyika.
Naye Daniel
Okoka ambaye ni makamo mwenyekiti wa ALAT msingi wa serikali kuu ni serikali za
mitaa hivyo kama serikali za mitaa hazitambuliki hakuna umuhimu wa kuwepo hata
hao viongozi wa ngazi hizo.
‘’ Kwa kuwa
kuna uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu , kama hawatatutambua katika
katiba basi tutasuasia uchaguzi huo ‘’ Alisema
Naye katibu
mkuu wa ALAT Habubakar Shamumoyo alisema
kuwa lazima kuwepo na vipengele
vinavyoelezea misingi, kanuni na masharti ya ung’atuaji wa madaraka kupeleka
kwa wananchi.
Alisema kuwa
kama alat ilitoa mapendekezo yake ili yaingie katika katiba hiyo lakini
hayakuzingatiwa na badala yake kimetamkwa kipengele kidogo.
0 comments:
Post a Comment