Pages

Subscribe:

Wednesday 5 February 2014

WANACHAMA WA CCM KAHAMA WAKATWA MAPANGA BAADA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KATA YA UBAGWE....MH KASULUMBAYI MBUNGE WA MASWA MASHARIKI NA WENGINE WASHIKILIWA NA POLISI KUHUSIKA NA UVAMIZI HUO.


Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro
Wanachama sita wa CCM akiwemo katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani Kahama wamejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa mapanga na kundi la watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana Majira ya sa moja jioni wakati wafuasi hao wa CCM wakitoka katika mkutano wa Hadhara wa kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Ubagwe wilayani Kahama....
katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa kabisa mkono wake wa kushoto
Waliojeruhuwa katika tukio hilo ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro ambaye amekatwa panga usoni.
Wengine ni katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa panga kichwani na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto na dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono
Pia amejeruhiwa Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi aliyejeruhiwa mguuni pamoja na Subira Nyangusu, huku ikielezwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo walipasua vioo vya gari la CCM na kuchukua funguo za gari hiyo.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wilaya ya Kahama, Andrew Emanuel majeruhi hao wamelazwa katika hospital ya wilaya hiyo, huku Kimaro, Masunga na Peter ambao hali zao ni mbaya wakipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
Imedaiwa katika tukio hilo wafuasi hao wa Chadema wamepora fedha zaidi ya shilingi milioni moja na laki tatu kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na simu za mkononi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amesema watuhumiwa 16 wa tukio hilo ambao ni wafuasi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilaya ya Kahama.
Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kahama
MBUNGE WA MASWA MASHARIKI SLYVESTER KASULUMBAYI ANAYESHIKIRIWA NA JESHI LA POLISI KUFUATIA VURUGU HIZO.

0 comments:

Post a Comment