Askofu wa jimbo katoriki la Morogoro Telesphori Mkude akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amazni naye alipata fulsa ya kuzungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa kata ya Kilakala akielezea jinsi walivyofarijika kupata kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bendera akiwa na viongozi wenzake katika picha ya pamoja.
Mkuu wa shirika la damu takatifu sista Claudia Maria akielezea historia ya kituo hicho.
Hii ni moja ya wodi ya wanaume katika kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizunguka kukagua mazingira ya kituo hicho
Wauguzi na wananchi wa eneo la jirani na kituo hicho wakifurahia katika uzinduzi huo.
Ulifika wakati wa kufungua muziki, viongozi hao waliondoka na miondoka ya mfano wa nyimbo za kabila la Kichaga wanaoshikana mikono .
Namie sikuwa mbali sanaa, hao wabibi nimekuwa nao tangu utoto wangu, tulikuwa tukisali pamoja katika kanisa la Kituo hicho, Tulikuwa wote katika Rejio Maria, nilifarijika sana nilipowaona nikaona niweke kumbukumbu.
Habari kamili soma hapa
ASKOFU wa jimbo Katoriki la Morogoro Teresphori Mkude
ameomba serikali kuwasaidia kuwaondolea kodi
kwa vifaa vya huduma za afya
wanavyoingiza ili waweze kuboresha zahanati na vituo vya afya katika
jimbo hilo.
Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha
St Thomas kilichopo kata ya Kilakala katika manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa wanafikiria zaidi kuboresha huduma ya afya
hususani vijijini na kwamba ili wafanikiwe
hakuna budi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kuwaondolea kodi hiyo.
Alisema kuwa tayari wameshaomba wafadhili kutoka nje
kwaajili ya kuwasaidia vitanda vitatu kwaajili ya kujifungulia wajawazito ili waweze kupeleka katika zahanati yao iliopo
Maskati Turiani wilayani Mvomero.
Pia aliomba serikali ya wilaya ya Mvomero kuwaboreshea
barabara ya kwenda Maskati ili iweze kufikika kwa nyakati zote na kuweza
kuwasaidia wagonjwa kufika katika zahanati hiyo kwa urahisi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa
Serikali inafarijika kuona mashirika ya dini yanapotoa huduma hizo ambapo aliwahakikishia kuwa nao bega kwa bega
katika kufanikisha huduma hizo.
‘’ Tangu miaka ya zamani mashirika ya dini ndio yaliweza
kutoa huduma bora zaidi za afya na elimu, na tunatambua mchango wenu ndio maana
hata mnapohitaji watumishi hatusiti kuwapatia’’ Alisema
Naye mkuu wa shirika la damu takatifu linalomiliki Kituo
hicho cha Afya sista Claudia Maria alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka
1982 kama zahanati ambayo ilikuwa ikitoa huduma
kwa wagonjwa wa nje .
Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa huduma hiyo kwa
wananchi wa manispaa ya Morogoro waliamua kuboresha na kukipandisha hadi hadi
kufikia kituo cha afya .
Alisema kuwa kwa sasa
wanampango wa kujenga chumba cha upasuaji ili wajawazito wanaopatwa na
matatizo waweze kupata huduma hiyo hapo.
Alisema kuwa kituo hicho kinahudumia wagonjwa 1074 kati ya hao 289 ni
wa mfuko wa bima ya afya na kuongeza kuwa changamoto walionayo ni mfuko huo kuchelewesha
malipo na kusababisha upungufu wa dawa .
0 comments:
Post a Comment