Pages

Subscribe:

Tuesday, 17 December 2013

MAMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WANAWAKE WA KIMATAIFA


MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA WANAWAKE AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA ASIA

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network, Bwana Tareq Ahmed Nizami, mwandaaji mwenza wa Mkutano wa  Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, 'The Africa -Middle East-Asia' unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The Palm, huko Dubai katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu (UAE), tarehe 16.12.2013. Mwandaaji mwingine wa mkutano huo ni Kituo cha Maendeleo ya Kiuchumi na Uongozi (CELD).
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa  wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika Dubai kuanzia tarehe 16.12.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania katika nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika katika hoteli ya Atlantis The Palm iliyopo Dubai, Jamhuri ya Falme za Kiarabu tarehe 16.12.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba, na wa kwanza ni Mshauri Maalum wa Mama Pohamba Mchungaji Justina Hilukiluah na wa mwanzo kushoto no Bwana Tariq Nizami, Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network.



 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasilisha mada ya Elimu: Key to the Future of Women in Emerging Economies, kwenye mkutano wa siku tatu wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika huko Dubai tarehe 16.12.2013.
 Mke wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba akimpongeza Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete baada ya kutoa mada iliyosisimua wajumbe wa Mkutano wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unafanyika jijini Dubai, Jamhuri ya Falme aza Kiarabu tarehe 16.12.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Mheshimiwa Margaret Zziwa, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki. Viongozi hao ni miongoni mwa viongozi wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wanaohudhuria mkutano wa siku tatu huko Dubai.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Dr. Angela Moore, Balozi wa Heshima kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani wakati wa mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia huko Dubai tarehe 16.12.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI

BABA NA MTOTO WAUWAWA NA RADI GEITA

SABA WAKAMATWA KWA MAUAJI YA MWENYEKITI WA ZAMANI WA CCM MKOA WA MWANZA

Marehemu Mabina alivyouawa
MWANZA, Tanzania
Watu saba wanashikiliwa na Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kinyama ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Clement Mabina.

Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofati wakiwemo wakazi wa maeneo ya Kata ya Kanyama yalikofanyika mauaji hayo na kundi la watu kwa kile kilichoelezwa kuwa mgogoro wa mashamba.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Valentino Mulowola, akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, alisema hadi sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na jana na kwmba jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya Mwenyekiti huyo wa Chama wa awamu iliyopita.

“Tunaendelea na upelelezi wa mauaji hayo ya kinyama nay a kujichuklulia sheria mkononi ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika na kuna maendeleo mazuri, tayari watu saba tunawashikilia kwa kuhusika na mauaji hayo,” alieleza Kamanda Mulowola

Katika tukio hilo la mauaji, Mabina aliuawa kwa kukatwa mapanga na kupigwa kwa mawe na mwili wake ulikutwa na majereha makubwa kichwani kisogoni.

Kabla ya kuawa na wananchi  hao, marehemu anadaiwa kumpiga risasi mtoto Temeli Malimi (12) kwa bahati mbaya wakati akijihami na mashambulizi ya wananchi hao.

Kamanda Mulowola alieleza jana kwamba, marehemu alikutwa akiwa na bunduki moja aina ya Shot Gun na bastola moja ambayo hakutaja aina yake.

Hata hivyo ndugu wa marehemu akiwemo msemaji wa familia Timoth Gregory, wanailaumu mitandao ya kijamii kwa kupotosha ukweli na kumpaka matope marehemu na hivyo kuomba waandishi wa habari waripoti ukweli na siki kuyafanya mauaji hayo kuwa mtaji wa kisiasa.

Habari kutoka katika eneo la tukio zimedai kuwa, mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa alikutwa na simu ya mkononi ya marehemu Mabina.
  
Habari hizo zimedai kuwa, kundi linalosadikiwa kuhusika na mauaji hayo lilijiandaa kufanya kitendo hicho cha kinyama kutokana na mvutano wa eneo la mlima huo. 

Kamanda huyo wa polisi hakutaka kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa madai ya kuwa kuyataja kungeweza kuvuruga upelelezi wa jeshi lake.  

Gregory alisema jana kuwa, taratibu za mazishi bado zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasubili watoto wawili wa marehemu walioko nje ya nchi.

VIONGOZI JUMUIA YA WAZAZI KINONDONI WAANZA SEMINA MOROGORO, CCM MORO WAMFAGILIA KINANA

 
 Mgeni rasmi, Dorothy Mwamsiku akiingia ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM Kinondoni, Charles Mgonja.
 Mgeni rasmi akiwa na viongozi wa Jumuia ya Wazazi na CCM, baada ya kuingia ukumbini
 Madenge akizungumza kabla ya semina kufunguliwa
 Dorothy akifungua semina hiyo
 Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini kwenye semina hiyo
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada kwenye semina hiyo
 Mmoja wa wajumbe akiwahamasisha wenzake baada ya semina kufunguliwa
Madenge akiagana na Dorothy baada ya semina kufunguliwa.

HABARI KAMILI

CCM MORO WAPONGEZA ZIARA ZA KINANA MIKOANI
*Mwenezi asema zianaimarisha, kujenga heshima ya chama
*Ataka Wana-CCM kuunga mkono ziara hizo 

BASHIR NKOROMO NA LATIFA GANZEL, MOROGORO
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimepongeza ziara za katibu mkuu wa CCM Abduraharam  Kinana kwamba ziara hizo zimezidi kukiimarisha chama na kukiongezea heshima.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku alisema hayo wakati akifungu semina ya viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM,  wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, leo, katika ukumbi wa Road View Motel iliopo Nane nane manispaa ya Morogoro.

Aliwataka wanachama wa CCM nchi nzima kumuunga mkono Kinana na Sektetarieti yake kwa kusimamia na kutekeleza maagiizo aliyotoa katika ziara hizo ikiwemo kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM na kisikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kusitatua.

Katibu huyo alisema kuwa kuna kila sababu ya viongozi wa CCM kutokubali kuwafumbia macho watendaji wanaoshindwa kutekeleza ilani ya CCM kwa makusudi kwa lengo la kukikwamisha chama hiki.

Alisema   kuwa wapo watendaji ambao hawakitendei haki chama cha  Mapinduzi kwa, kufuja  fedha za miradi kwa makusudi .

'' Unakuta baadhi ya watendaji hawatekelezi ilani ya CCM ipasavyo na hivyo kusababisha CCM kusemwa vibaya, tusikubali, sisi tuwe wakwanza kuwashughulikia kabla ya sisi kunyoshewa vidole'' Alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kuna kila sababu kwa viongozi wa CCM na wanachama kwa ujumla wanatambua miradi yote ya maendeleo iliopo ktika maeneo yao inavyoanza kutekelezwa ili ikitokea mtendaji anafanya ubadhilifu iwe rahisi kuwashughulikia.

Aidha alisema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za baadhi ya watendaji wanaokwamisha utekelezaji huo wa ilani lakini  hadi sasa ilani hiyo imetekelezwa kwa kiasi kikubwa.
"Pamoja na utekelezaji huo bado wapo watu wanaosema CCM haijafanya kitu, kazi ya wapinzani kukosoa  na CCM kazi yatu kutenda, tusikate tamaa tusonge mbele.

Aliwataka jumuiya ya wazazi kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto kwa kuwa hiyo ndio moja ya malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo badala ya kuwaachia vijana wakiharibika na kutumbukia katika vitendo viovu vinavyopelekea kupata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Kwa upende wake Mwenyekiti wa CCM wilaya Kinondoni, Salumu Madenge ambaye ndiye Mwenyekiti wa semina hiyo, alisema,  lengo la semina hiyo ni kuwaweka viongozi hao katika mazingira ya ulelewa wa kutosha wa namna mbalimbali ya kutekeleza majukumu yao na wajibu wa kwa chama cha Mapinduzi.

Awali mwenyekiti wa wazazi wilaya ya Kinondoni Charlse Mgonja alisema  katika semina hiyo mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo umuhimu wa mchango wa jumuiya hiyo katika kuimarisha chama cha Mapinduzi, na historia na kusimamia maadili ya wanachama na viongozi ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya CCM na jumuiya zake.

Monday, 2 December 2013

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTOHUBIRI CHUKI

VIONGOZI wa dini mbalimbali nchini wametakiwa kutohubiri chuki na badala yake wahubiri amani na utulivu bila kujali mitazamo ya mathehebu tofauti.

Sunday, 1 December 2013

HONGERA BENDERA

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akiwa ameshikilia kifimbo alichokabidhiwa na wafugaji wa jamii ya Masai  kama moja ya zawadi baada ya kutunukiwa shahada ya udaktari.

CHELEKO CHELOKO NA VIFIJO KWA DOCTA BENDERA

 Katika sherehe za kutunukiwa shahada ya (Docta of Philosophy in Humanity) kutoka chuo kikristo cha Calfornia State cha Nchini Marekani CSCU RC Bendera na Ole Medeye jana katika viwanja vya Ikulu ndogo.

KUANZIA LEO UTAITIKA KWA JINA LA RC DK BENDERA

RC Bendera akitunukiwa shahada rasmi ya  (Docta of Philosophy in Humanity) kutoka chuo kikuu cha  kikristo cha Calfornia State cha Nchini Marekani CSCU.

SASA NI DAKTARI RC JOEL BENDERA



Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera na Naibu waziri Ole Medeye wakisubiri kutunukiwa shahada ya (Docta of Philosophy in Humanity) kutoka chuo kikristo cha Calfornia State cha Nchini Marekani CSCU.

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MOROGORO AKIONGOZA MAANDAMANO


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Inocent Karogeries akiongoza maandamano ya sherehe ya kutunukiwa shahada ya (Docta of Philosophy in Humanity) kutoka chuo kikristo cha Calfornia State cha Nchini Marekani CSCU mkuu wa mkoa wa Morogoro joel Bendera na Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na makazi Ole Medeye jana katika viwanja vya Ikulu ndogo mkoani hapa.

WANAWAKE OYEEEEEEEEEEE


Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Morogoro Mariam  Kiamani akifungua  baraza la UWT Novemba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Veta Morogoro

WANAWAKE LAZIMA WAWEZESHWE MAFUNZO, SAWA MHESHIMIWA MNEC.

Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akiteta jambo na katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli wakati wa kikao cha baraza la UWT mkoa wa Morogoro Novemba 29 mwaka huu Veta Morogoro

WAJUMBE WA UWT KATIKA KIKAO VETA MOROGORO


Wajumbe wa UWT mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano wa baraza hilo lililofanyika Novemba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Veta Morogoro.