Wema Sepetu.
TAARIFA ikufikie kuwa chanzo cha Mkurugenzi wa Endless Fame Productions, Wema Isaac Sepetu kutimua baadhi ya wafanyakazi wake akiwemo dairekta wake ni ufuska uliokubuhu huku magari yake yakigeuzwa gesti au danguro.‘NI TOO MUCH’
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema alifikia hatua hiyo hivi karibuni ili kuficha skendo hiyo kubwa kwa sababu ilikuwa ‘too much’.
Ilifahamika kuwa pamoja na Wema kumpenda dairekta huyo kiasi cha kumwachia magari yake kutokana na ubunifu wake na uchapaji kazi lakini ilifika mahali akamshindwa.
“Alimpa uhuru wa kufanya kila kitu ikiwemo kutumia magari yote kama kiongozi wa kampuni,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kweli jamaa alikuwa anatanua kila mahali. Mara Uhuru Peak, mara Coco Beach akiwa na totozi.
COCO BEACH, KINONDONI
“Kuna siku, moja kati ya magari ya Wema lilinaswa pale ufukweni Coco Beach likinesanesa na baada ya muda alishuka mwanamke akijitengenezatengeneza nguo zake.
“Ukiacha hiyo kuna siku nyingine lile jeusi lilinaswa maeneo ya Kinondoni ambapo mabinti walikuwa wakipishana kuingia na kutoka.”
TAARIFA MEZANI KWA WEMA
Ilielezwa kuwa habari za magari yake kutumika kwa ufuska zilimfikia Wema ambaye alimtimua dairekta huyo na wenzake waliokuwa wakitumia magari hayo ‘kung’olea’ watoto wazuri.
“Wema ana mashabiki sana hivyo wakiona magari lake wanadhani ni yeye ‘so’ wakijichanganya tu wanaingia wenyewe kwenye kumi na nane za washikaji na kujikuta wakiwafaidisha,” kilisema chanzo. Ilidaiwa kuwa ilifika hatua wasichana wa mjini wakayajua magari yote ya Wema, jambo ambalo ni hatari kwani staa huyo anaweza kuvamiwa na kuhatarisha maisha yake.
Lakini ili kunusuru yote hayo ndipo Wema akafikia hatua ya kuchukua uamuzi huo mgumu.WEMA ANASEMAJE?
Katika kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimsaka Wema lakini hakupatikana kwa njia zote badala yake alipatikana mratibu wa shughuli zote za kampuni hiyo, Petit Man ambaye alisema: “Yaah…ni kweli ishu hiyo imetokea. Unajua mwanzoni bosi alikuwa akiambiwa tu na watu kuwa magari yake yanatumika ndivyo sivyo ‘so’ alipojiridhisha ndiyo akachukua uamuzi huo ili kunusuru ‘imeji’ ya kampuni.”
Source: GPL
0 comments:
Post a Comment