Pages

Subscribe:

Sunday, 31 August 2014

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MOROGORO, AFANYA MAJUMUISHO NA WATENDAJI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris  alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Gairo ya kwenye kikao cha majumuisho na watendaji wa mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa wa Morogoro
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla

Friday, 29 August 2014

KIKWETE ATAKA WAZEE WAINGIZWE KWENYE MFUKO WA BIMA YA AFYA ,ILI KUONDOA MALALAMIKO YA KUNYANYASIKA KWAO.

 Rose Ongara meneja mfuko bima ya afya Morogoro akikabidhi mashuka  220 kituo cha afya cha  Gairo kwa Rais Jakaya Kikwete wakati alipotembelea kituo hicho juzi.
Wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Kikwete, na viongozi mbalimbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la  Gairo Ahmed Shabiby, mkuu wa  wilaya ya Gairo Khanifa Karamagi, mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Mtei.

habari zaidi soma hapa chini,






 RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa mfuko wa bima ya afya kwa wananchi na kutaka wazee waingizwe kwenye mfumo huo ili kuepuka kunyanyasika.

Alisema hayo jana wakati wa majumuisho  ya ziara yake yaliofanyika wilayani Gairo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi katika wilaya zote sita za mkoa wa Morogoro.

‘’ Nendeni mkajifunze kule Kilindi wenzenu walifanya ujuzi gani wa kuwaingiza wazee katika mfumo wa bima ya afya, kwa sasa  malalamiko kwa wazee kwa wilaya ile hakuna tena’’ Alisema.

Alisema kama wilaya zote ziatafanikiwa kufanya hivyo malalamiko ya wazee kudharauliwa wakati wakihitaji matibabu  tutakuwa tumeyamaliza kabisa.

‘’ wazee wenyewe sio wengi kama watu wanavyotafsiri, watu wote tupo milioni 48, tuliozaliwa kabla ya muungano ni milioni 4 tu ambao ndo wazee sasa ni wengi hao tushindwe kuwahudumia’’ Alisema.

Alisema mfuko huo unasaidia sana katika suala zima la matibabu kwa kuwapatia huduma watu tegemezi 4 kwa kiasi cha shilingi 10,000 jambo ambalo ni dogo ukilinganisha na matibabu bila mfumo huo.





Wednesday, 27 August 2014

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

 : Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
 Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

Tuesday, 26 August 2014

JK ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014.
2
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.
3
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014.

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. 

Sunday, 24 August 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MJINI MOROGORO, AWATAKA VIONGOZI WAACHE WOGA KUSIMAMIA SHERIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi 
mradi mkubwa wa maji ambao  umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014

Saturday, 23 August 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE UZINDUA JENGO JIPYA LA SACCOS

Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata  utepe  kuzindua jengo jipya la Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha kijiji cha Kinole, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014. Wengine ni Mama Salma Kikwete (kulia),  Mbunge wa Viti Maalum Dkt Lucy Nkya (wa [ili kulia) na Mwenyekiti wa SACCOS ya Kinole Mzee Issa Ramadhani Kambi

RAIS KIKWETE ATAWAZWA KUWA CHIFU MSAIDIZI WA WALUGURU NA CHIFU KINGALU HUKO KINOLE, MOROGORO, APEWA JINA LA CHIDUKILA

 CHIFU wa Waluguru Kingalu
Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha “muibukaji”, kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.
 CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumvika mgolole Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014

Friday, 22 August 2014

RAIS KIKWETE ASAFIRI KWA TRENI YA TAZARA KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipanda treni ya TAZARA kuelekea Kisaki Mkoani Morogoro akiwa katika ziara yake ya mkoa huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera, Mbunge wa Morogoro Kusini  Mhe Innocent Kalogeris na KAtibu wa Rais Bw. Prosper Mbena wakiongea ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki mkoani Morogoro.

RAIS KIKWETE AWEKA AFUNGUA KITUO CHA AFYA KIBAONI, MOROGORO VIJIJINI


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Wabunge Mhe Abdul Mketeme (kushoto) na Mhe Getrude Rwakatale (kulia) wakifunua pazia kwa pamoja kuashiria kufungua kituo cha Afya cha Kibaoni Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.

Thursday, 21 August 2014

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KILOMBERO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia wananchi kwa furaha wakati akielekea ukingoni mwa Mto Kilombero kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero Agosti 20, 2014. Anaoongozana nao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (kushoto) na Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais)
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kudumu juu ya mto Kilombero  Agosti 20, 2014. Pamoja naye ni  Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuri (kushoto kwa Rais), Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki Mhe. Celina Kombani (kulia), Mbunge wa  Mama Salma Kikwete (nyuma ya Rais), Mbunge wa Ulanga Magharibi Dkt Haji Ponda (kulia) na Mbunge wa Kilombero Mhe Abdul Mteketa (kulia kwa Rais)

Sunday, 10 August 2014

VIJANA 30 KUTOKA AFRIKA KUSINI WALIOZURU MORO WAFURAHIA UHURU WA NCHI YA TZ

Vijana 30  wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini wakiwa katika eneo la dakawa ilipokuwa kambi ya  ya waliokuwa wapigania uhuru katika eneo la dakawa wilayani Mvomero, ambao walifika nchini kwaajili ya kujifunza historia ya uhuru wao kama njia moja ya kuazimisha miaka 20 ya uhuru wa Kidemokrasia.
 Timu ya waandishi wa habari kutoka Afrika Kusini waliokuwa katika ziara hiyo.

 mmoja wa vijana hao akiwa katika moja ya darasa katika shule ya sekondari ya Dakawa.

 Mratibu wa Ziara hiyo Bwana Magesa akiongoza safari ya vijana hao kutoka katika eneo la Magadu ambako nako kuna historia ya wapigania uhuru hao.

 Vijana hao wakiwa katika kujadili baada ya kutembelea eneo la Magadu manispaa ya Morogoro.


 Vijana 30  wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini wakiwa katika makaburi ya waliokuwa wapigania uhuru katika eneo la dakawa wilayani Mvomero, ambao walifika nchini kwaajili ya kujifunza historia ya uhuru wao kama njia moja ya kuazimisha miaka 20 ya uhuru wa Kidemokrasia.

Waandishi wa habari wakiwa katika eneo la Magadu mjini hapa.

Moja ya mambo ambayo vijana hao wamefurahishwa nayo ni pamoja na uhuru wa nchi ya Tanzania,

Vijana hao kwa nyakati tofauti walikuwa wakishikwa na mshangao kuona wananchi wa Tanzania jinsi wanavyoweza kutembea kwa uhuru masaa yote bila ghubudha yeyote.

walidao nchini kwao huwezi kutembea na kitu cha thamani barabarani bila kupata  msukosuko wowote vinginevyo uwe unajulikana sana.

walisema mara nyingi vitu kama simu na laptop huvitumia wakiwa nyumbani na kisha kutembea hivi hivi.

Pia walifurahia elimu inavyotolewa kwa gharama ndogo hapa nchini ukilinganisha na nchini kwao.

Walishangazwa na watanzania waliozaliwa na raia wa nchi yao kutaka serikali yao kuwasaidia uraia wa nchi hiyo sambamba na elimu jambo ambalo haliwezekani.
walidai hakuna elimu inayotolewa bure na kwamba kila raia wa nchini kwao ni lazima afanye jitiada za kutafura riziki na kwamba sio wanapata bure kama ambavyo watu wengine wanadhania.
Pia walisema suala la kuwepo kwa watoto hao halihusu serikali yao na kwamba hayo yalikuwa ni makubaliano na watu na watu na sio ya nchi,
walisema kwa kipindi baada ya kupatikana kwa uhuru watoto hao walikuwa na maamuzi ya kuchagua kwenda na wazazi wao au kubakia Tanzania.
walisema kwa sasa kutaka nchi hiyo kuwapa uraia ni sawa na kutafuta marumbano na nchi ya TZ ambayo watoto hao ndio raia wake.


WAZIRI KOMBANI ATAKA WAKULIMA KUFUFUA VYAMA VYA USHIRIKA

. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani amewataka wakulima kusahau yaliopita juu ya vyama vya ushirika na kuvifufua kwani ndio mkombozi wao, Alisema hayo wakati wa kuhitimisha kilele cha siku ya wakulima 88 mkoani Morogoro.
 
 Kombani akisindikizwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq, pamoja na mwenyekiti wa TASO kanda ya Mashariki Mohamed Mzee ,a katibu wake Rafael kumtunza mwana dada huyo aliyekuwa kivutio cha burudani katika maonyesho hayo baada ya kupiga danadana kwa zaidi ya nusu saa bila mpira kumponyoka.

 Mkuu wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka akiwa katika moja ya bada linalozalisha mahindi ya lishe lijulikanoalo kama CPP Tanzania Co.LTD, Mtaka ni miongoni mwa wakulima wa mbegu hiyo mkoani Morogoro, baadhi ya wananchi walimwambia Mtaka kwamba ameonyesha kipaji chake kuwa  ni kilimo na kumtaka kuwashawishi viongozi wengine kuiga mfano wake, 
'' Mimi ni mkulima, nimeanza kuonyesha kipaji changu, sio kusubiri hadi ustaafu ndio unaanza kutafuta cha kufanya,'' alisema Mtaka.

 Mahindi yaliotumika kuonyesha mfano katika banda hilo yanatoka katika shamba la Mkuu huyo wa wilaya ya Mvomero Mtaka ambayo amelima wilayani humo.

 Viongozi wa wilaya ya Kilombero wakiwa katika maonyesho hayo siku ya kilele cha 88 mkoani Morogoro.

 Maafande wa JKT kanda ya mashariki wakipokea zawadi ya ushindi wa kampuni za zana za kilimo ambapo wamenyakua nafasi ya kwanza.
 Makamo mkuu wa chuo kikuu cha kilimo SUA Profesa Monella akipokea zawadi baada ya kushika nafasi ya kwanza katika kilimo na utafiti.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro akiwa katika maonyesho hayo na viongozi wengine mkoani hapa.
 Msanii kutoka wilaya ya Bagamoyo akionyesha fani yake kwa kuigiza kujikata panga ambalo lilionekana kuingia mwilini pasipo kutokwa na damu.

Wasanii kutoka Mtibwa wakionyesha burudani ya sarakasi kwa kutumia viti vulivyopangwa juu ya chupa za bia.