Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha kuwezesha vijana kielimu na kiuchumi SOMAFCO , TLHOLO Mohlathe akimwonyesha Naibu waziri wa elimu ya juu ya Afrika Kusini Mduduzi Manana eneo ambalo wapigania uhuru walitumia kama ofisi zao.
Huo ni ujumbe wa wanavyuo 30 kutoka Afrika Kusini waliotembelea kampasi ya Mazimbu SUA Morogoro kuangalia kumbukumbu za wapigania uhuru wa nchi yao .
Wanavyuo hao wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri huyo katika eneo lililokuwa la kiwanda cha samani katika kampasi ya Mazimbu.
Wanafunzi hao wakiwa katika ziara ya kutembelea katika kampasi ya SUA
Naibu waziri huyo akiangalia kwa makini maeneo hayo ya kumbukumbu za wapigania uhuru.
habari zaidi soma hapo chini.
NAIBU Waziri
w a elimu ya juu nchini Afrika Kusini Mduduzi Manana jana amejikuta katika mazingira magumu baada ya vijana walioachwa na wapigania uhuru
pamoja na wakimbizi wa nchi hiyo, kumvaa na kutaka kuwapa majibu ya hatima yao
juu ya suala la elimu.
Sintofahamu
hiyo ilimkuta waziri huyo wakati alipokuwa akitembelea eneo kilipokuwa chuo cha
wapigania uhuru wa Afrika kusini cha
Solomoni Mahalangu (SOMAFCO) ambacho sasa ni kampasi ya chuo kikuu cha kilimo
SUA.
Mery Twala ni
mmoja wa watoto kati ya 80 walioachwa na wakimbizi hao waliokuwa wakiishi Mazimbi
manispaa ya Morogoro, ambao kwa sasa
wanaishi eneo la Dark Cite pamoja na mama zao
ambapo wengine wamefiwa na wazazi wao wote wawili.
‘’Tumechoka
,mnakuja na kutulisha chakula tuu bila
kuelewa hatima yetu katika elimu’’ alisema kwa sauti ya juu mtoto huyo.
Alisema wao walizaliwa watatu na kwamba baada ya
kupatikana kwa uhuru wan chi hiyo baba yao aliondoka na kaka na dada yake huku
akimwacha yeye na mama yake ambaye kwa sasa ameshafariki dunia.
Alisema
ameshindwa kupata elimu sahihi kutokana na mazingira magumu kwani mama zao
walikuwa wafanyakazi wa ndani wa wapigania uhuru hao hivyo baada ya kuondoka
kazi na masomo ya watoto hao havikuendelea.
‘’ Mimi siwaelewi hawa watu kila mwaka
wanakuja lakini hawatutatulii matatizo yetu, wanajua baba zetu waliondoka na
kutuacha tunasoma lakini tuliachishwa na na kushindwa kuendelea na shule,,
alisema
Vijana hao
kwa pamoja waliitaka Serikali hiyo kutoa
tamko rasmi kama haiwatambui ili wajue kuwa wao ni watoto wa mitaani na yatima.
Kilio cha
vijana hao kilimgusa waziri huyo na kusema Serikali yake haita kaa kimya na
itahakikisha inatatua tatizo hilo kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Hata hivyo
Naibu waziri huyo alisema ugeni huo haukuja kwa masula hayo na kwamba kutoa majibu ya moja kwa moja
itakuwa ngumu kwake na kuahidi kulifikisha suala hilo mara atakapurudi nchini
kwao.
Naye Anna
Mngoni aliishushia lawama serikali hiyo kwamba waliwaahidi baada ya kupata uhuru watarudi ili kuja
kuwalipa mafao ya wastaafu lakini hadi sasa ni miaka 20 imepita hakuna mwelekeo
wowote.
‘’ Mimi ni
mstaafu wa ANC, walipoondoka tulistaafishwa kazi, lakini hadi sasa hatujalipwa,
wenzetu wengine walishakufa, nasie ni
wafu watarajiwa, tunataka kujua hatma ya
malipo yetu’’ alisema.
Hata hivyo
Waziri huyo alisema kwa kuwa serikali hiyo iliahidi suala hilo ni lazima
lishughulikiwe na kuwataka kuvuta subira ili nalo aweze kuliwasilisha ili kuweza kutolea majibu sahihi.
Naibu waziri
huyo kabla ya kuongea na wanajumuiya ya SUA , mamia ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM , na watoto hao
alitembelea makaburi ya wapigania uhuru na wakimbizi katika kampasi ya mazimbu na kuweka mashada.
Afrika kusini inatimiza miaka 20 tangu kupata
uhuru wa Kidemokrasia, imeamua kuleta vijana 30 kutoka vyuo vikuu vya nchi hiyo
kutembele mazimbu moro ili kujua
historia ya nchi yao.
0 comments:
Post a Comment