Michael Mayalla mwenyekiti
kitongoji cha Majichumvi akiongea katika mkutano wa pamoja na wananchi wa kitongoji hicho, waliokutana kujadili madai ya kuporwa mashamba yao yanayodaiwa kupewa vigogo.
Mwananchi huyo alikutwa aneo hilo la maji Chumvi akiteka maji , ambapo alidai kuna changamoto ya maji sambamba na uchafuzi wa maji hayo unaofanywa na wafugaji,
Habari zaidi soma hapo chini,
Mgogoro unatokana na maafisa ardhi kuanza zoezi hilo zaidi ya mwezi mmoja sasa bila kutoa taarifa ama elimu yoyote kwa uongozi wa kijiji hicho juu ya nini wanachofanya.
Michael Mayalla mwenyekiti kitongoji cha Majichumvi alisema hayo juzi wakati wa mkutano wa pamoja na wananchi wa kitongoji hicho waliota kujua hatma yao juu ya mashamba hayo.
‘’Tunashangaa kuona watu wa ardhi wanakuja kupima mashamba yetu huku wakijua kuna wakulima na wafugaji walihamishiwa humo kwa zaidi ya miako 10 iliyopita’’alisema
Mwenyekiti huyo alisema maafisa hao wa ardhi wakiulizwa juu ya suala hilo wamekuwa wakitoa kauli za vitisho kwa wakazi hao , wakidai mashamba hayo yanamilikiwa na vigogo.
Afisa ardhi wa wilaya ya Mvomero Majaliwa Jafari alisema kati mwaka 1980 hadi 1990 serikali ilitenga ekari 60,000 za mashamba kwa ajiri ya kilimo cha nguvu kazi katika kijiji hicho.
Hata hivyo alisema baadhi ya mashamba yalinunuliwa na baadhi ya watu ambapo mengi hawakuendelezwa.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali ilitoa agizo kuyatambua mashamba pori ili yaweze kufutwa na kuangalia nini cha kufanya.
Mgogoro unajitokeza ,ni sitofahamu kwa wananchi waliohamishiwa humo na wanaoishi zaidi ya miaka 10 sasa ambao ni wakulima na wafugaji zaidi ya 1000 baada ya serikali kuanza zoezi la ukaguzi na upimaji wa mashamba hayo bila taarifa kwao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Wami Luhindo Apolinali Kahumba anasema katika kijiji chake kuna vitongoji 6 ambapo Maji chumvi ni miongoni mwa vitongoji hivyo.
Alisema kinachofanyika ni Halmashauri kutowashirikisha kama uongozi wa kijiji na kwamba hata pale walipopeleka maombi yao ili waweze kujua ni eneo lipi ambao wananchi wanapaswa kutumia kumekuwa hakina majibu sahihi.
Alisema kwa mujibu wa sheria vijiji vina mamlaka ya kugawa eneo lake kupitia mkutano mkuu wa kijiji na kwamba kama serikali inahitaji eneo ni lazima kijiji kishirikishwe.
0 comments:
Post a Comment