Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Amelazimika Kuhairisha Bunge Jioni Hiii mara baada ya Kutokea Vurugu.Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katika Jaji Joseph Sinde Warioba Alitakiwa kuwasilisha Rasimu ya Pili katika Bunge Hilo.Wajumbe wa Bunge Walipoingia Ukumbini Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Mh Samwel Sitta Alipomwita Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mh Jaji Warioba ,
Monday, 17 March 2014
MAUAJI YA KUTISHA : MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA NA PANGA SHINGONI.
Na Mwandishi wetu,Geita yetu Blog
WIKI moja baada ya Tanzania kuungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake duniani,kauli mbiu ikiwa ni "chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia" mkoani Geita hali imekuwa tofauti baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Modester Shija (55-60) mkazi wa kitongoji cha Kamlale,kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani hapa kuuliwa kikatili kwa kukatwa mapanga Machi 14,mwaka huu na watu wasiojulikana.
WIKI moja baada ya Tanzania kuungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya wanawake duniani,kauli mbiu ikiwa ni "chochea mabadiliko kuleta usawa wa kijinsia" mkoani Geita hali imekuwa tofauti baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Modester Shija (55-60) mkazi wa kitongoji cha Kamlale,kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani hapa kuuliwa kikatili kwa kukatwa mapanga Machi 14,mwaka huu na watu wasiojulikana.
Sunday, 16 March 2014
ANGALIA AJIRA MPYA KUTOKA JESHI LA POLISI
TANGAZO LA AJIRA JESHI LA POLISI ,MACHI 2014
KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI KWA WAHITIMU WATARAJIWA WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2014 na kidato cha nne mwaka 2013. Ili kutekeleza azma hii tumeweka fomu kwenye tovuti ambayo wahitimu watarajiwa wa kidato cha sita wa mwaka 2014 watajaza kabla ya kufanya mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita. Baada ya kujazwa kikamilifu wakabidhi fomu kwa wakuu wa shule ambao watazirejeshe kwa Makamada wa Polisi wa mikoa kabla ya tarehe 17.03.2014. Wahitimu wa kidato cha nne wasijaze fomu hizi walishajaza kupitia “selform” walizojaza walipokuwa shuleni.
ANGALIA MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA
Kutoka Kalenga Kunakofanyika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo hii leo. Matokeo ya AWALI nikama Ifuatavyo 
CCM kura 451,CHADEMA 261 NA CHAUSTA 2
CCM kura 451,CHADEMA 261 NA CHAUSTA 2 ANGALIA MAJINA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA
MITAA (OWM - TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA
MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14.
A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI INATANGAZA ORODHA
YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA
IFUATAVYO:-
i. Walimuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za
vyuo vyaualimu Tanzania Bara.
B: Kila Mwalimu ( Ajirampya) atatakiwakuzingatiayafuatayo:-
1. Kuripoti
tarehe01/04/2014kwenyeofisizaWakurugenziwaHalmashaurikwaajili
yakupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
Saturday, 15 March 2014
ANGALIA PICHA MTIBWA SUGAR WATOKA SARE YA BILA KUFUNGANA NA YANGA
Waliosimama Kutoka Kushoto : Salum Mbonde,Dickson Daud,Abdalah Juma, Ally Shomary, Shaban Nditi,Walioinama Kutoka Kushoto : Vicent Barnabas, Said Mkopi,ShabanKisiga,Husein Ramadhan, Paul Ngalema
Kikosi cha Timu ya Yanga Kilichoanza Leo : Kutoka Kushoto Didier Kavumbangu, Haroub Canavaro,Khamis Kiiza,Oscar Joshua,Frank Domayo,Simon Msuva, Juma Abdul,Nizar Khalifan,Mbeleni Juma Kaseja.
Ligi Kuu Tanzania Bara Imendelea Leo Ambapo Katiak uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Kulikuwa na Mchezo Mkali Dhidi ya Wenyeji Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Mkoani Morogogo Dhidi ya Mabingwa Watetezi Yanga ya Dar es Salaam . Katika Mchezo Huo Hadi Dakika 90 za Mchezo Zinamalizika Matokeo Timu Hizo Zmetoka sare ya Bila Kufungana.Mchezo Ulikuwa Mkali na wakukamiana Pamoja na Hali ya Uwanja Kutokuwa nzuri kutoka na Mvua Zianzoendelea Kunyesha Mkoani Hapa.Timu ya Yanga walitengeneza Nafasi Nyingi za Kufunga lakini walishindwa Kuzitumia .Wachezaji Emanuel Okwi na Didie Kavumbangu walipata nafasi za kufunga katika dakika ya 80 na 88 lakini awalishindwa kufunga, Yanga walifanya Mabadiliko katika Dakika ya 65 Alitoka Nizar Khalifan na Kuingia Said Dilunga,Dk78 Alitoka Khamis Kiiza na Kuingia Husein Javu.
Mtibwa Sugar Walipata Pigo katika Dakika ya 70 Ambapo Mshambuliaji Wao Abdalah Juma Alionyeshwa Kadi Nyekundu kwa Kumchezea Rafu mbaya.
Friday, 14 March 2014
MBUNGE WA MORO KUSINI ALILIA FIDIA ZA WANANCHI WAKE KIDUNDA
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogeries akiongea kwenye warsha ya siku moja ya wadau kujadili taarifa ya tathimini ya athari za kijamii na mazingira ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere hadi Kidunda pamoja na mtambo mdogo wa kuzalisha umeme na njia ya umeme kutoka Kidunda wilaya ya Morogoro hadi Chalinze , warsha hiyo imefanyika katika hotel ya kitalii ya Nashera mjini hapa.
Muu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecksadik akiongea juu ya mafanikio ya mradi huo wa maji katika miko ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, ambapo amesema wananchi wa Dar wanatumia zaidi ya lita peke yake wanatumia lita milioni 450 kwa siku.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiongea wakati wa warsha hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha hiyo ambapo alisisitiza jinsi ya utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa wingi katika mikoa hiyo ili kuepuka kutumia maji ya visima ambapo mengine hutumia gharama kubwa kuyatibu.
Katibu mkuu wizara ya maji mwandisi Bashir Mrindoko akiongea wakati wa warsha hiyo.
Mwenyekiti wa badi ya DAWASCO Eva Sinale akiongea wakati wa warsha hiyo
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifutilia kwa makini ufunguzi wa warsha hiyo.
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa makini kufutilia warsha hiyo.
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Inocent Kalogeries ameitaka Serikali kuharakisha malipo ya fidia ya wananchi wa eneo linapotarajia kujengwa bwawa la maji la Vidunda ili kuondokana na kero hiyo.
Alisema hayo wakati wa warsha ya kujadili taarifa ya tathimini ya athari za kijamii na mazingira ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere hadi Kidunda na mtambo wa kuzalisha umeme na njia ya umemem kutoka kidunda hadi Chalinze .
Alisema kuwa mpaka sasa kuna kero hiyo kwa wananchi wake na kwamba wanakosa majibu wao kama wanasisas juu ya fidia za wananchi hao.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na umuhimu wa bwawa hilo atahakikisha anawashawishi wabunge wa mikoa ya Dar, Pwani na Morogoro kuhakikisha wanapigania bajeti ya maji kuongezwa ili kusaidia ujenzi huo na fidia za wananchi hao kwa haraka.
Katibu mkuu Muhandisi Bashiri Mrindoko alisema kuwa fidia kwa wananchi hao ni bilioni 3.6 ambapo alidai kuwa ujenzi wa bwawa na barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe pamoja na umeme huo utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 160.
Subscribe to:
Posts (Atom)













