Pages

Subscribe:

Monday, 12 May 2014

VIZEE VINAVYOKIUKA MISINGI YA MWALIMU NYERERE VISIENZIWE; MWIGURU

 Naibu katibu mkuu wa CCM Mwiguru Nchemba akipokelewa wilayani Gairo alipokwenda jana kwa ziara yake ya siku moja  wilayani humo.

 Nchemba akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Gairo.

 Nchemba alipowasili katika ofisi ya CCM wilaya ya Gairo ambapo alikutana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya mkutano wa hadhara.

 
 Mkuu wa wilaya ya Gairo Khanifa karamagi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ialani kwa Nchemba katika kikao cha kamati ya siasa.

 Nchemba wakati akielekea katika mkutano wa hadhara

 Nchemba akisalimiana na wananchi wa Gairo waliofurika katika mkutano huo


 Mwiguru akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.

 Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akizungumza kabla ya kumkaribisha mwiguru katika mkutano wa hadhara Gairo.


Awali Mwiguru alipowasili katika ofisi za CCM akivalishwa skafu. 

habari zaidi soma hapa


NAIBU katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Mwiguru Nchemba amesema wazee wanaofuta misingi ya kudumisha amani na utulivu wanchi alioacha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wataheshimiwa na kuenziwa na chama hicho na kwamba wale wanaokiuka wabezwe kwani hawana nia njema na nchi.

Mwiguru   ambaye pia ni naibu waziri wa fedha alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani Gairo ambapo alifanya mkutano wa hadhara kuzungumzia kero kubwa ya maji inayokabili wilaya hiyo.

‘’ Wazee wote ambao wanafuata misingi ya baba wa taifa kudumisha amani na utulivu wan chi CCM itawaheshimu na kuwaenzi, lakini wale ambao wakati baba wa Taifa alikuwepo wakawa wanajificha kwa unafiki wao na sasa wameona kuwa hayupo wajitokeze na kutaka kuvuruga amanni na utulivu tulionao hatuwawafumbia macho’’ Alisema

Alitolea mfano mmoja wa wazee hao ni Jaji Warioba ambaye alipewa heshima ya kukusanya maoni ya katiba na kazi hiyo alishakamilisha lakini cha kushangaza bado kila kukicha anakaziania kuwepo kwa Serikali tatu jambo ambalo kamwe CCM halitakubali.

‘’ Huyo mzee ni waajabu kweli, alipewa kazi ya kusimamia ukusanyaji wa maoni ya katiba lakini sasa kila kukicha unamwona kwenye vyombo vya habari akililia serikali tatu, hana nia njema na serikali yetu , msimamo wa CCM ni serikali mbili tuu’’ alisema

Aliwataka vijana kutambua kuwa serikali tatu ni mzigo ambao haubebeki na kwamba watakaoumia ni watanzania kwa kuongezewa kodi mara dufu ya hivi sasa.

‘’ Kwa sasa tunahangaika kutafuta ajira kwa vijana, hizo fedha za kuendeshea serikali tatu badala ziende kwenye mambo ya maendeleo na  ili vijana waweze kupata ajira ‘’ alisema
Alisema kuwa kwa sasa  kwa sasa pato la taifa ni tririoni 7.7 na kati ya hizo tririoni 4 zinatumika kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi  na zilizobakia ndio fedha za maendeleo.

‘’ Sasa hii serikali ya tatu ikija hizi fedha za maendeleo ndio ziachuhudumia huko na kwamba fedha za maendeleo tutegemee kwa wafadhili hiyo inaingia akilini kweli? Alihoji

Hata hivyo alisema watahakikisha inakuwepo sheria  itakayosimamia fedha za mfuko wa vijana ambazo zitakuwa zinatoka moja kwa moja  badala ya kupitia katika mifumo mingine ambapo mara nyingi imekuwa ikikwamisha.

Alifafanua na kusema  upo utaratibu wa kila halmashauri kutoa fedha za mfuko wa vijana ambao kwa asilimia kubwa hazifikii walengwa kama ilivyokusudia na kwamba sheria hiyo itasaidia kubana mfumo huo na hivyo fedha kufikia vijana moja kwa moja.




Wakati huo huo alisema
NAIBU waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba ametangaza vita dhidi ya matajiri wanaokwepa kodi kwa kushirikiana na mawakala  na watumishi wa Serikali na kwamba ameomba kupewa taarifa ili aweze kupambana nao.
Mwiguru alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani Gairo mkoani Morogoro alipokwenda kusikiliza kero ya maji kwa wananchi wa wilaya hiyo.
‘’ Tunaingia rasmi kwenye vita ya wakwepa kodi, kama kuna mawakala, watumishi  wanaoshirikiana na matajiri hao tupeni taarifa ili tuwashughulikie, hatuwezi kuzoza kodi kwa wauza vitumbua huku matajiri wanakwepa kodi’’ Alisema
Alisema wanaandaa sheria ya kufuta misamaha kwa ya kodi kwa watu ambao hawastahili sambamba na kuweka sheria bitakayosimamia kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi.
‘’ Wapo matajiri ambao ikiwekwa kodi wanawatumia wananchi kulalamikia ili wafutiwe kwa kigezo cha kutokuwa na uwezo, sio watanzania wote hawana uwezo ambao labda ukiweza kodi kwenye simu washindwe kulipa, mbona milio ya simu wanakwatwa fedha lakini hawalalamiki , hii tumeshaibaini na sasa tutaishughulikia’’ Alisema
Hata hivyo alisema kuwa wanaangalia  uwezekano wa kupekela sheria ya usimamizi mzuri wa fedha za Serikali .
Kwa upande mwingine Mwiguru aliwatoa hofu wananchi wa Gairo atahakikisha wanapatiwa visima vya maji vya muda wakati wakisubiri mradi mkubwa  unaofadhiliwa na benk ya dunia ambao kwa sasa unasuasua kutokana na kuwepo na maji ya chumvi katika yvanzo vilivyokusudiwa kwaajili ya mradi huo.
Alisema kwa sasa amepata taarifa kuna maji yanayotoka katika mto uliopo jirani na mradi huo na kwa kuaznia watatumia kiasi cha shilingi milioni 300 za fedha za ndani kupata visima hivyo huku juhudi za kuhakikisha chujio la kuchuja maji ya chumvi zinaendela kufanyika.
Alisema tatizo la maji  ni ajenda tofauti na inatakiwa kushughulikiwa na kupewa uzito wa kipekee na kwamba isihusishwe na masuala ya kisiasa kama ambavyo wapinzani wamekuwa wakitumia mwanya huo kwa sasa.
Alisema serikali inatambua umuhimu wa maji kwa wananchi wake na ndio maana hata katika bajeti ya mwaka huu fedha nyingi zimeelkezwa katika miradi ya maji ili kuhkikisha wananchi wanaondokana na dhana hiyo.

 

Tuesday, 6 May 2014

WABUNGE WAPYA WAAPISHWA LEO

Spika wa Bunge Anna Makinda
 







Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo linaanza kikao chake cha Bajeti, ambapo muda wa kuchangia na kuwasilisha bajeti za wizara mbalimbali, umepunguzwa.


Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, alisema muda wa kuchangia Bajeti hiyo, umepunguzwa kutoka dakika 10 hadi saba na muda wa uwasilishaji wa bajeti za wizara mbalimbali, pia umepunguzwa.
Alisema kutokana na mabadiliko hayo, sasa kila wizara itapewa siku moja ya kuwasilisha bajeti yake na kujadiliwa. “Tumepima muda tukaona unatosha,“ alisema.

WAZIRI AAGIZA KIWANDA CHA NGUO KITUMIE MITAMBO YA KUCHEMSHA MAJI YA MAKAA YA MAWE NA SIO YA NAYOTUMIA KUNI


 WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith Malenge  alipotembelea kiwanda cha Twenty Firts Centuary kuangalia matumizi ya makaa ya mawe badala ya magogo ya miti waliokuwa wakitumia zamani na kupigwa marufuku na serikali.


 Waziri huyo akiangali maeneo mbalimbali ya mabwa ya maji katika kiwanda  hicho.







 Waziri huyo akiangali maji yanayotoka kiwandani humo ambayo yanakemikali yanaingia katika mto Ruvu ambayo yanamadhara kwa binadamu.






WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith Malenge amekiagiza kiwanda cha Twenty first centuary kuhakikisha ifikapo mwezi Agosti mwaka huu wawe wamebadilisha mfumo wa maboiler ya kutumia nishati ya magogo ya miti na kuingia katika mfumo wa makaa yam awe.
Alisema hayo jana wakati alipotembela kiwandani hapo kuangalia jinsi ya uendeshaji wa kiwanda na kujionea mfumo mzima wa uhifadhi wa mazingira kiwandani hapo.
Alisema kuwa pamoja na juhudi walizofanya kiwanda hicho kuacha kutumia magogo ya miti ambayo yalikuwa yakiharibu mazingira na kuingia katika mfumo wa makaa ya mawe lakini bado mfumo wa vifaa  vya kuchemshia maji upo katika mfumo wa kutumia magogo.
Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa vumbi linalosambaa hewani na hivyo kusababisha kero kwa wananchi wa maeneo jirani na hapo.
‘’ sasa ni lazima ikifika mwezo wa nane mbadilishe maboiler yenu yawe katika mfumo wa makaa yam awe ili kuondokana na usumbufu’’ Alisema Waziri huyo.
Hata hivyo waziri huyo alishauri faini zinazotozwa na NEMC zingetumika kuboresha mabwawa ya maji yanayotumiwa na viwanda vya nguo na ngozi vya mjini hapa ili kuweka mazingira safi.
‘’ Mimi naona hizi faini mnazotoza mngezipeleka kuhakikisha mnaboresha mabwawa hayo ili kuondokana na adha ya maji kujaa  na kufurika nje ya mabwawa na kusababisha adha kwa wananachi wa karibu na  hata kuingia mtoni na badae kuleta madhara kwa watumiaji wa mto huo ‘’ Alisema
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi alipongeza juhudi zilizofanywa na vyombo vya habari mkoani hapa za kuhakikisha wanaripoti btaarifa juu ya matumizi ya magogo ya miti kwa kiwanda hicho hadi kufikia sasa matumizi hayo yamechwa.
‘’ Kweli serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya habari  kuhakikisha zoezi la matumizi ya  magogo limesitishwa sasa’’ alisema Amanzi.

WAZIRI GHASIA AWAKALIA KOONI WANAOTUHUMIWA KWA RUSHWA KATIKA UHAMISHO WA WALIMU

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia  akioongea na wajumbe wa baraza la wizara hiyo wakati wa kujadili bajeti ya wizara yake uliofayika jana mjini hapa





 Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakisikiliza kwa makini mkutano huo wa baraza jana

 Wajumbe wa baraza hilo .


Habari zaido soma hapo chini


Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia amesema  upangaji wa vituo kwa watumishi wapya hususani walimu ni eneo moja wapo lenye hafuru ya Rushwa  na kutaka watumishi wanaotuhumiwa kuchukuliwa hatua.

 Alisema eneo hilo limeanza kutoa dalili si njema na kuongeza kuwa ni vyema wakachukua tahadhari na kujiridhisha kwa kubaini mapungufu ya kiutendaji katika eneo hilo na kuhakikisha wanaziba mianya ya rushwa.

Alisema hayo Mei 5 mwaka huu wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa TAMISEMI linaoendela mkoani Morogoro.

Aidha alimuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuchukua hatua za haraka  dhidi ya watumishi  wanaotumiwa kwa rushwa au kutoa huduma kwa upendeleo na wale wanaoshirikiana na maafisa katika mamlaka za serikali za mitaa kuzihujumu mamlaka hizo.
Waziri Ghasia alisema ofisi hiyo imepigiwa kelele kwa muda mrefu na wadau mbalimbali  juu ya vitendo vya rushwa,hivyo ni wakati sasa kwa wizara hiyo kuchukua hatua madhubuti za kuboresha mifumo ya
‘’ Ni muda muafaka sasa kuhakikisha tuhuma hizo zinakwisha, kwa kuchukua hatua madhubuti za kuborsha mifumo ya utendaji kazi katika eneo hili’’ Alisema

Alisisitiza juu ya kuimarisha usimamizi na ufutiliaji wa matumizi ya fedha  kupitia MSM  kupitia mifumo ya fedha waliokwishawekeza (Epcor/IFMS) ambapo alisema dalili zinaashiria ufuatiliaji kupitia mifumo hiyo bado ni hafifu.

Katibu mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne  Sagini aliwataka watumishi wa ofisi hiyo    kujadili changamoto zinazoikabili ofisi hiyo ili ziweze kutatuliwa na waweze kufanya kazi kwa ufanisi.

Kikao cha baraza la wafanyakazi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa kinafanyika mjini Morogoro na kimelenga kujadili bajeti ya wizara hiyo kabla ya kwenda kujadiliwa kwenye bunge la bajeti mjini Dodoma.


Saturday, 3 May 2014

WAANDISHI WA HABARI MSIKUBALI KUTUMIWA, UNGANENI

  • DSC_0341
Mwanahabari Mkongwe kutoka Chuo Kikuu Huria, Dokta Samwilu Mwaffisi (kulia) akiwasilisha mada ya Maadili ya Uandishi wa Habari kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Bw. Simon Berege.
DSC_0311
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda (wa pili kushoto), akitoa maoni yake wakati wa kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0310
Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya, akishiriki kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
DSC_0281
Baadhi ya washiriki wakichangia maoni yao kwenye kongamano la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha. (Picha na Zainul Mzige) (FS)

BULEMBO ALIA NA WANAOTENGENEZA MARAIS KABLA YA MUDA, ASEMA WATASHUGHULIKIWA

 Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa Abdalla Bulembo akizindua Website ya jumuiya hiyo Mkoa wa Morogoro.

 Hiyo ndio muonekano wa website hiyo baada ya kuzindulika jana.

 Bulembo akisalimiana na  wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili katika hotel ya Nashera jana ambapo baraza hilo lilifanyika.



Viongozi wa jumuiya ya wazazi wakiwa katika picha ya pamoja eneo la Tungi wakisubiri kumpokea mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya hiyo.


Habari zaidi soma hapa.





MWEMYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdallah Bulembo amewaonya viongozi  wa jumuiya hiyo  kuacha tabia ya kujihusisha na utengenezaji wa makundi ya Urais,Wabunge na madiwani ndani ya chama hicho  muda wa kampeni haujafika.

Alisema  kwani kufanya hivyo kunasababisha kuwepo na mpasuko na hivyo kushindwa  kutekelezaji  ilani ya chama hicho.

Bulembo alitoa onyo hilo jana wakati akifungua mkutano mkuu wa baraza la wazazi Mkoani hapa ambapo alisema kuwa chama hicho hakina makundi na kwamba kundi lao ni moja ambalo kiongozi wake Rais Jakaya Kikwete.

Bulembo alisema chama hicho kina utaratibu wa kuwapata viongozi wake kwa vikao na kwamba kiongozi anayetakiwa kuungwa mkono ni Yule atakayechaguliwa na CCM muda na wakati ukifika.

‘’ Mwanachama au kiongozi yeyote atakayebainika kufanya hivyo hatutasita kumchukulia hatua’’ Alisema.

Hivyo aliwataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao ya kuboresha jumuiya ya wazazi kuanzia ngazi ya chini ikiwa ni pamoja na kuwajibika katika kufanya kazi na kuacha kuwakatisha tamaa viongozi ambao bado wako madarakani.

Akizungumzia suala la katiba mwenyekiti huyo alisema kuwa msimamo wa chama chake ni kuwa na serikali mbili ambazo zilikuwepo kwa miaka 50 na kwamba zimedumu ndani ya muungano.

Hata hivyo alisema kuwa suala la muugano ni la watanzania wote hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuudumisha ikiwa ni pamoja na  kufanya marekebisho ya changamoto zilizopo ambapo alisema kuwa ndani ya miaka 50 kumekuwepo na marekebisho mengi ambayo yamefsnyika.
Hivyo aliwataka watanzania kuendelea kuutetea na kuulinda muungano huo mpaka mwisho.

Kwa upande wake katibu wa wazazi Mkoa wa Morogoro Shaweji Mkumbula alisema kuwa jumuiya hiyo inakabiliwa na changamoto ambazo jumuia hiyo inaendelea kuzifanyia kazi .

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kutofanyika kwa vikao katika ngazi ya chini kwa mujibu wa kanuni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama kadi kanuni DCR pamoja na usafiri kwenye baadhi ya maeneo ya Wilaya.

Nyingine ni Viongozi ngazi ya kata na matawi kushindwa kuhamasisha wanachama kulipa ada zao kwa kuzingatia maelekezo ya kanuni.

Ufunguzi wa mkutano huo ulienda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya jumuiya hiyo pamoja na ugawaji zawadi kwa Wilaya zilikamilisha ujenzi wa Ofisi ya wazazi ambapo Wilaya ya Morogoro iliibuka mshindi na hivyo  kujishindia  kombe pamoja na zawadi ya sh.laki 3