Waziri wa ulinzi Dk Husein Mwinyi akiangalia samani zinazotengenezwa na shirika la Mzinga la mkoani Morogoro kwaajili ya matumizi ya shule, ofisi na nyumbani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 40 ya shirika hilo.
Dk Husen Mwinyi akimpatia cheti cha kutambua mchango wake mmoja wa wafanyakazi waanzilishi wa shirika hilo.
Kikundi cha burudani cha shirika la mzinga wakiwa katika sherehe hizo baada ya kutumbuiza.
Wafanyakazi na familia za wanajumuiya ya shirika la Mzinga wakiwa katika viwanja vya sherehe hizo juzi.
Waziri Mwinyi akisalimiana na mkuu wa majeshi Devis Mwamunyange baada ya kuwasili katika bwalo la jeshi la Magadu manispaa ya Morogoro.
Dk Mwinyi akiweka jiwe la msingi katika eneo la Magadu linapojengwa jengo la kituo cha utafiti na ulengaji wa silaha.
Waziri huyo akipata maelezo ya jinsi mashine ya kutengeneza matofali ya njanja iliotengenezwa na shirika hilo.
Mkuu wa majeshi Mwamunyange, na waziri Mwinyi wakibadilishana mawazo katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya shirika la Mzinga, kulia ni meneja wa shirika hilo Meja Jenerali Dk Charles Muzanila.
Mkuu wa majeshi Mwamunyange akipata maelezo ya ujenzi wa nyumba maalum za kulala wageni zinazojengwa katika eneo la Bwalo Magadu sambamba na bwawa la kuogelea la kimataifa ujenzi utakaogharimu kiasi cha sh milioni 700
habari zaidi.
WAZIRI wa ulinzi Dk Husein Mwinyi, ameliagiza shirika la Mzinga
la Mkoani Morogoro kuhakikisha wanatengeneze zana zote za kijeshi ili kupunguza
gharama kwa Serikali kuziagiza nje ya nchi.