Pages

Subscribe:

Tuesday 16 September 2014

MBARONI KWA KUBAKA NA KUSABABISHA KIFO MORO





KIJANA mmoja  Jumanne Husein (18) mkazi wa Nemela  Mkuyuni wilaya ya Morogoro, anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kubaka mtoto wa miaka 4 na kumsababishia kifo chake.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard  Paul alisema tukio hilo lilitokea Septemba 7 mwaka huu  saa 2.00 usiku  huko Mkuyuni.

Kamanda huyo alisema mama wa mtoto huyo  Rehema Juma Rashid alikuwa amekwenda katika shughuli za kijamii, na kumwacha mtoto  sebuleni, ambapo mtuhumiwa huyo aliingia na kumbaka.

Alisema mama  huyo aliporudi alimkuta mtoto akiwa na  maumivu  makali,  na alipofutilia aligundua kufanyiwa kitendo hicho na kijana huyo.

Alisema baba mlezi wa mtoto huyo  Uledi Mabange (30)mkazi wa  Nemela Mkuyuni, alikuwa akimshawishi mama huyo kukubaliana kinyemela ili suala hilo lisifike kwenye vyombo vya sheria jambo.

Hata hivyo kamanda huyo alisema ilipofika Septemba 13 mwaka huu majira ya asubuhi mtoto huyo alifariki dunia.

Alisema kufutia tukio hilo Polisi wanamshikilia baba mlezi huyo pamoja na mtuhumiwa wa ubakaji huku wakiwatafuta watu wengine waliokuwa wakishawishi kesi hiyo isifike kwenye vyombo vya sheria.

Alisema mtuhumiwa wa ubakaji alikiri kufanya tukio hilo na kwamba anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment