habari zaidi soma hapo chini
MTU mmoja
Salvatory Maganga maarufu kwa jina la Nionzima raia wa Burundi ,anashikiliwa na
polisi baada ya kupatikana na vitu mbalimbali vya kufanyia matukio ya ujambazi.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, mtu
huyo alikamatwa Agosti 31 mwaka huu saa 10.30 katika eneo la Makaburini Mjimpya mansipaa ya Morogoro.
Kamanda huyo
alisema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na Raia
wema , walibaini mtu huyo kuwa anamiliki
vifaa hivyo na kuamua kumwekea mtego na hatimaye kumkamata.
Alitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na kifaa
kilichotengenezwa na vyuma mithiri ya
misumari maalumu kwaajili ya kutegea magari barabarani.
Alisema vitu
vingine ni visu 10, turubai, darubini, nyaya kufanyia milipuko na bauruti pamoja
na mkanda maalumu wa kuvaa tumboni unaosaidia kufanya milipuko hiyo.
Pia alisema
mtu huyo alikutwa na kitambulisho cha kupigia kura cha hapa nchini na hati ya
kusafiria ya nchini Burundi ambayo inaonyesha miaka ya kuzaliwa tofauti.
Alisema mtu
huyo baada ya kufanyiwa mahojiano ya
awali alidai alitengeneza vitu hivyo kwaajili ya kutega magari barabarani ili
aweze kupata riziki kutokana na maisha yake kuwa magumu.
Hata hivyo
kamanda huyo alisema polisi wanaendela na uchunguzi wa kina kujua nia ya rais
huyo kukutwa na vitu hivyo hatarishi
Wakati huo huo
JESHI la
polisi mkoani hapa limefanikiwa kumkatama
Hashim Ngalawi (39) mkazi wa Mang’ula wilayani Kilombero akiwa na
bunduki aina ya mark4 na meno ya tembo mawili.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa Leonard Paul alisema mtu huyo alikamatwa Agosti 31 mwaka huu,
saa 10.45 usiku huko Kanono kisawasawa wilayani Kilombero.
Kamanda huyo
alisema mtu huyo anashiliwa na polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya
uchunguzi kukamilika.
Wakati huyo
huo Leonard Gaspa anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kumporea bastola meneja wa kiwanda cha tumbaku .
Alisema tukio
hilo lilitokea Agosti 30 mwaka huu majira ya uskiu wa manane katika eneo la
Kahumba manispaa ya Morogoro.
Akielezea
mazingira ya kuporwa bastola hiyo kamanda huyo alisema, ilitokea purukushani baina ya watu hao wawili
wakiwa ndani ya gari ambapo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kupora bastola hiyo
na dola za Kimarekani 700 na kasha kutoweka
nazo.
Alisema mtuhumiwa
huyo alikutwa akitumia dola hizo katika baa mbalimbali mjini hapa na
kwamba hadi anakamatwa alikutwa na dola
mia moja tu.
Alisema polisi
wanaendela na uchunguzi juu ya tukio hilo na kwamba atafikishwa mahakamani mara
baada ya uchunguzi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment