Pages

Subscribe:

Friday, 7 February 2014

MANGULA ASEMA MITANDAO YOTE YA KAMPENI ZA URAIS WAMESHAIBAINI WATAISHUGHULIKIA

 Makamo mwenyekiti wa CCm Taifa Philipo Mangula akivishwa skafu na chipukizi baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Morogoro.

 Makamo mwenyekiti huyo akisalimiana na mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro Juliana Mwenda.
makamo huyo akisalimiana na katibu wa UVCCM mkoa wa Morogoro Nicodemas.
 Makamo huyo akiongea na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro pamoja na wa wilaya ya Morogoro mjini.

Hayo ni mapokezi aliopata alipoingia  katika kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa

Mangula akifungua shina la wakereketwa la Njia panda katika kata hiyo ya Rudewa
 Maelfu waliofurika katika kata hiyo wakati wa kampeni ya udiwani ya Rudewa.
 Mangula akiwa na mgombea wa udiwani kata ya Rudewa Subiri Joseph.

Habari zaidi soma hapa chini.

MAKAMO Mwenyekiti  wa chama cha Mapinduzi Taifa Philipo Mangula amesema kuwa muda wa kampeni  za Urais,udiwani, ubunge na hata nafasi za serikali za mitaa bado   na kwamba wanaofanya kampeni wanakiuka katiba na kanuni na hivyo  CCM inatambua mitandao yote na itawashughulikia.
Alisema hayo Februari 8 mwaka huu wakati akiongea na viongozi wa wilaya na mkoa wa Morogoro alipofika kwajili ya kampeni  za Uchaguzi mdogo  wa udiwani katika kata za Ludewa wilayani Kilosa na Tungi Manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa tayari walishafungua mafaili ya watu hao wenye mitandao ya kampeni na kwamba wanatambua mitandao yote hata katika ngazi za mikoa na watawashughulikia.
Alisema kuwa Rais, wabunge na madiwani waliopo madarakani   bajeti yao ya mwisho  inashia mwezi Juni 2015  na kwamba wanaojitokeza sasa ni waharifu na lazima wachukuliwe hatua.
 Aidha alisema kuwa Viongozi waliopo madarakani wanahaki zote na kwamba ni lazima walindwe ili waweze kufanya kazi zao vizuri bila kunyanyasika na kwamba kuanza kampeni hizo kunafanya kuwavunja nguvu viongozi hao.
‘’Mara zote tatizo la kuanzisha makundi kabla ya kampeni ni kusababisha chuki na uhasama na kupelekea makundi hayo kurushiana maneno, na hiyo inasababisha hata nchi kushindwa kutaalika’’ Alisema
Aliwataka viongozi kutengeneza mitandao ya kuwafutilia watu hao wenyekufanya kampeni za chini kwa chini kinyume na taratibu na kukabiliana nazo .
‘’ Ni mwiko kwa mtu kuunda vikundi na kufanya kampeni za chini kwa chini , tutakabiliana nazo’’ alisema.
Alisema kuwa suala la kutangaza nia ya kutaka kugombea nafasi yeyote sio kosa bali kuanza kampeni ndio kosa kubwa kimaadili ya chama.
Kwa upande mwingine Mangula alisema kuwa wabunge na madiwani kufanya zaira za mara kwa mara ni sawa na mkulima kupalilia shamba lake hivyo wanaodharau kufanya hivyo wasije kulaumu na kwamba watavuna walichopanda.
‘’ Ni dhambi kubwa  kwa mbunge kutotekeleza ahadi  zake, ni sawa na mkulima kupanda mbegu pasipo kufanya palizi, akikuta mazao yake yameliwa na magugu atamlaumu nani’’ Alisema.
Kwa upande mwingne Mangula alisema kuwa nia ya mwenyekiti wa CCm taifa Rais jakaya Kikwete ni kuhakikisha katiba inakamilika haraka  ili itumike katika uchaguzi ujao.
Alisema kuwa itakuwa vema ndani ya siku 70 zilizopangwa kwaajili ya bunge la katiba ikakamilika na kurejeshwa kwa wananchi  ili kutimiza malengo yaliokusudiwa.
Awali katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi walionuna baada ya majina walioyataka kurejeshwa katika uchaguzi huo kutorudi na hivyo kususia kampeni  jambo ambalo Mangula alisema kuwa si dhambi kurejeshwa kwa mgombe wa nafasi ya 3 kinachozingatiwa ni vigezo.
Pia alisema kuwa katika kata ya Ludewa wananchi wake wanalalamikia mbunge wao Mustapha Mkulo kutotimiza ahadi alizoahidi.




ANGALIA MAJINA YA WAJUMBE WATAKAOSHIRIKI KATIKA BUNGE LA KATIBA WATAJWA JIONI HII IKULU DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

UTANGULIZI

1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na 
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu 874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:



Na.
Kundi/Taasisi
Taasisi zilizoleta mapendekezo
Idadi ya Watu Waliopendekezwa
Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa
Idadi ya Walioteuliwa
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
Tanzania Bara
Zanzibar
1.
Taasisi zisizokuwa za Kiserikali
246
98
1,203
444
20
13
7
2.
Taasisi za Kidini
55
17
344
85
20
13
7
3.
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
21
14
129
69
42
28
14
4.
Taasisi za Elimu
9
9
84
46
20
13
7
5.
Makundi ya Walemavu
24
6
97
43
20
13
7
6.
Vyama vya Wafanyakazi
20
1
89
13
19
13
6
7.
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
8
1
43
4
10
7
3
8.
Vyama vinavyowakilisha Wavuvi
7
3
45
12
10
7
3
9.
Vyama vya Wakulima
22
8
115
44
20
13
7
10.
Makundi yenye Malengo Yanayofanana
142
21
613
114
20
14
6

Mapendekezo Binafsi
-
-
118
-




Jumla
672
178
2,880
874
201
134
67

Jumla Kuu
850
3,754









8. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.

9. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.


WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAKUTANISHA WADAU KUTOA MAONI KUHUSU MIKATABA YA UTENDAJI KAZI KATIKA TAASISI ZA UMMA

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano wa wadau kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Mkutano huo uliandaliwa mahsusi ili wadau waweze kufahamu mambo muhimu juu ya Mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi hususan chimbuko, maana na faida zake, mambo ya msingi yatakayofanikisha utekelezaji wa mfumo huo, fomu ya mkataba wa utendaji kazi na vipengele vyake, vigezo vya upimaji wa utendaji kazi wa taasisi, wahusika wa mikataba na utaratibu wake; utaratibu wa kutoa taarifa za mikataba ya utendaji kazi, utaratibu wa kutathmini mikataba ya utendaji kazi; utaratibu wa kushindanisha Taasisi za Umma; na Taasisi zinazopendekezwa kuingia katika Mikataba ya Utendaji Kazi . Sambamba na hilo wadau walipata fursa ya kutoa maoni, ushauri na mapendekezo juu ya mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi, na namna bora ya kuitekeleza katika Taasisi za Umma. Wadau walioshiriki mkutano huo ni pamoja na watendaji na watendaji wakuu wastaafu katika Taasisi za Umma wakiwemo Makatibu Wakuu wastaafu, watendaji wakuu wa Asasi za Kiraia (AZAKI), wanataaluma kutoka vyuo vya Elimu ya juu, wawakilishi kutoka katika sekta binafsi na Washauri waelekezi Wanaojitegemea.

Thursday, 6 February 2014

48 MBARONI KWA KUFUNGA BARABARA YA MOROGORO NA IRINGA

 Wakazi wa doma wilayani Mvomero wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji kuondolewa eneo hilo.



WATU 48 wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kufunga barabara ya Morogoro na Iringa wakishinikiza wafugaji wa jamii ya Kimasai kuhamisha katika eneo la Doma wilayani Mvomero.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Februari 6 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi.
Kamanda huyo alisema kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kuwatia mbaroni wanawake 24 na wanaume 24 ambao wanadaiwa kufanya vurugu hizo.
Alisema kuwa fujo hizo zilitokea baada ya watu hao kudai kuwa wafugaji hao waliwapiga na fimbo wananchi wenzao waliokwenda porini kukata mkaa jambo lililowafanya nao kuamua kufunga barabara hiyo.
Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa walifanikiwa kufungua barabara hiyo majira ya saa 7 mchana baada ya kupiga mabomu ya mchozi kwa lengo la kuwatawanya wananchi hao.
Alisema kuwa hakuna madhara yeyote ya kibinadamu yaliotokea ingawa watu hao walijaribu kuwapiga mawe polisi hao .
Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kwamba watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kesho ili kuweza kujibu tuhuma hizo.
Kwa upande wao wananchi hao wamalalamikia wafugaji hao kitendo chao cha kuingiza mifugo mashambani na kuharibu mazao njambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Pia walilalamikia uongozi wa kijiji hicho cha Doma kwa kuwaingiza wafugaji kinyemela hali inayofanya kuwa wengi huku eneo la malisho likiwa dogo hali inayofanya wafugaji hao kuingiza mifugo yao mashambani.
Ibrahim Ndegalo alisema kuwa mbali na wafugaji hao kuwapiga lakini pia wamakuwa wakiwanyang’anya mali zao bila sabababu na kwamba maisha yao yamekuwa hayana amani.

NI DHANA POTOFU KUWA SHULE ZA KATA HAZINA UBORA

 Cheti cha mwanafunzi Petter aliyeshinda mashindao ya Nsha Afrika Mashariki kilichotolewa na manispaa ya Morogoro kama motisha kwa lengo la kuwatia moyo wanafunzi wanaofanya jitihada katika masomo yao.
 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Ali naye ni mshindi wa shindano hilo kwa SADEC ambaye amekuwa mshindi wa pili na kupewa 50,000 na cheti.
 Huyo ndiye Petter mwenyewe kutoka shule ya sekondari ya kata ya Tushikamane ambaye ni mshindi wa shindano hilo kwa Afrika Mashariki ambaye amepatiwa cheti na shilingi 200,000

Watendaji katika Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.


Baada ya kupokea zawadi hiyo Petter aliomba serikali kuziangalia shule za kata kwa kuzipatia walimu wa masomo ya sayansi wa kutosha  pamoja na maabara.
Alisema kuwa shule nyingi za kata zinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na walimu wa masomo ya sayansi pamoja na walimu wa masomo hayo.
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha dhana potofu kuwa shule za kata hazina ubora na badala yake watambue ukuwa ubora wa elimu unatokana na juhudi binafsi za wanafunzi wenyewe.
Alisema kuwa siri ya kushinda kwake kumetokana na juhudi binafsi alizofanya kutafuta material kutoka sehemu mbalimbali pamoja na kushirikiana na walimu.
Alisema kuwa imefika wakati kwa wanafunzi kutobweteka na kuanza kuelekeza juhudi binafsi katika masomo kwa kutafuta material mbalimbali hata nkatika mitandao

FINCA KUSAMEHE MADENI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DUMILA

 Meneja wa FINCA Ben Mwanyapu akikabidhi msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko katika kambi ya Magole wilayani Kilosa na kuahidi kuwafutia madeni waathirika hao,

 Afisa afya wa mkoa wa Morogoro Lymo akionyesha kichanja cha kuhifadhia vyombo ili kuepuka magonjwa mbalimbali kwa wahanga hao
 Wanafunzi waliofika katika godauni la mkoa la kuhifadhia chakula cha msaada katika eneo la dakawa kwaajili ya kupata msaada huo

Baadhi ya waathirika wa mafuriko wakiwa katika foleni ya kusubiri

Habari zaidi soma hapa chini


KAMPUNI ya fedha ya FINCA tawi la Morogoro  imesema inawafutia deni la zaidi ya milioni 30 zilizokopwa na wanachama wake ambao walipatwa na Mafuriko wilayani Kilosa mkoani hapa ili waweze kujipanga na kukopa tena kwaajili ya kuendelza biashara zao.
Meneja wa kampuni ya FINCA tawi la Morogoro Ben Mwanyapu alisema hayo jana wakati alipotembela kambi  ya waathirika wa mafuriko hayo katika eneo la Magole wilayani Kilosa na kutoa msaada wa unga wa mahindi na maharage  yenye thamani ya shilingi milioni 1.2.
Alisema kuwa kwa sasa wanachofanya ni kuhakiki wanachama hao na kwamba taratibu hizo zikikamilika watafanya zoezi hilo.
Aliwataka waathirika hao kujipanga upya kwaajili ya shughuli za kujikwamua kiuchumi badala ya kukataa tamaa kutokana na mafuriko hayo yaliowatia hasara kubwa.
Hata hivyo aliwahakikishia wanachama hao kuwa akiba zao zipo hivyo watazitumia kwaajili ya kukopa mikopo yao  hiyo.
Aliwataka kuwa wavumilivu  katika kipindi hiki kigumu na kwamba janga hilo sio liwafanye wakate tamaa ya maisha na badala yake wafikirie jinsi ya kujikwamua na kurudia katika hali yao ya zamani.
Kwa upande wao waathirika hao walishukuru kampuni hiyo kwa kuwathamini na kuwasamehe deni hilo ambalo lilikuwa ni mzigo mzito uliotokana na kuzolewa kwa mali zao zote zikiwemo biashara zao.
‘’ Tulikuwa tunafikiria jinsi gani tutalipa fedha hizo, maana mitaji yetu yote imeondoka na maji, lakini sasa tumeingia na matumaini mapya’’ Alisema Joseph Simoni.
Kwa upande wao wanawake waliopo katika kambi hiyo wamalalamikia kukosa haki yao ya msingi ya kupata unyumba kutokana na kulala kwa jinsia moja na hivyo kushindwa kulala na waume zao.
‘’ Kwa kweli hali hii ni ngumu kweli, wanaume zetu wanakuwa wakali, wakija wanakukalipia nipikie uji, kumbe tatizo ni tendo la ndoa, na wakati mwingine tunalazimika kufanya tendo la ndoa usiku machakani hali ambayo inahatarisha maisha yetu,, Alisema Asha Mohamed.
Naye afisa maendeleo ya jamii wa wilaya  ya Kilosa alisema kuwa kwa sasa chakula wanachopata kinawasaidia kudumua kwa siku 34 hvyo tatizo la chakula sio kubwa.
Aliomba  wasamalia wema wanaoweza kuwasaidia misaada pia wasaidie aina tofauti za mboga kama dagaa ,chumvi na mafuta  ili wahanga hao waweze kubadilisha mlo


MABOMU YA MACHOZI YATUMIKA KUWATAWANYA WAKULIMA MELELA, MOROGORO


Askari wa Kikosi cha kutuliza Fujo Akizima  Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa Leo Asubuhi.Wakulima hao walifunga Barabara hiyo kwa Lengo la kushinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Joel Bendera  Ili kutatua Mgogoro uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopo katika vijiji hivyo.Askari wa jeshi la Polisi walilazimika Kutumia Mabomu ya Machozi mara baada ya Wananchi wao kugoma Kuonana na Kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Mvomero Ikiongozwa na Mkuu Wa Wilaya ya  mvomero