Pages

Subscribe:

Saturday, 26 July 2014

MKUU WA MKOA MORO AONGOZA MAMIA KUMZIKA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI.

 Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wa staafu na watu mashuhuli wamefulika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro CCM >>>

Thursday, 17 July 2014

MAJAMBAZI SITA WAKAMATWA MORO

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paulo akionyesha moja ya silaha zilizokuwa zikitumika katika matukio ya ujambazi, ni baada ya kukamata majambazi  wanne na kuwatia nguvuni.


Habari zaidi soma hapo chini.



WATU  sita   wanashikiliwa na polisi mkoani hapa , watatu kwa tuhuma za ujambazi na wengine wawili  tuhuma za ujangili.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard Paulo aliwaambia waandishi wa habari  jana ,  kukamatwa ka majambazi na majangili  hao kumetokana na  oparesheni maalumu iliofanywa na jeshi hilo.

Kamanda huyo alisema kuanzia Juni 16 hadi Julai 3 mwaka huu jeshi hilo liliendesha oparesheni hiyo na kufanikikiwa kuwakamata waharifu hao na silaha mbalimbali.

Aliwataja majambzi hao Saidi Salehe (30) mkazi wa Kilosa,  Alayazi Makweya (30) mkazi wa Ludewa na Abdul Mateo maarufu  kama baba Ubaya mkazi wa Turiani Mvomero.

Alisema majambazi hao walikamatwa wakiwa  na bunduki aina ya AK 47 ikiwa na risasi 3  kinyume na sheria.

Hata hivyo kamanda huyo alisema Jeshi hilo pia lilifanikiwa kumtia nguvuni jambazi ambaye tayari aliwahi kufungwa miaka 10 kwa makosa  ya ujambazi.

Kamanda huyo alisema jina la jambazi huyo lime hifadhiwa kwa sababu ya wanaendelea na uchunguzi zaidi na kwamba alikamatwa eneo la Mikumi wilayani Kilosa.

Kamanda huyo alisema Julai 16 mwaka huu jeshi hilo liliwakamata majangili wawili Ayoub Abeid  maarufu  Mkwenejele (36) mkazi wa Kilosa  na Nassoro Mohamed maarufu kwa jina la Kambala.

Kamanda huyo alisema majangili hao walikamatwa katika eneo la Mzombe Tarafa ya Mikumi wilyani Kilosa  baada ya polisi waliokuwa katika oparesheni hiyo kuwatilia mashaka watu hao walikuwa wamevalia makoti makubwa meusi.

Alisema watu hao walikuwa na pikipiki namba T 630 BVH SunLg  na kamba baada ya kuwapekuwa wakuwakuta na silaha aina ya Riffle namba AO48441 na risasi 13   bila kibali cha kumuliki silaha hiyo.

Alisema vitu vingine walivyokutwa navyo majangili hao ni unga na samaki pamoja na mazni wa kupimia bidhaa ambao walikuwa wakiutumia kwa kupima wanyama hao baada ua kuwakamata.

Alisema watuhumiwa hao walipohojiwa walisema wamekuwa wakifanya  shughuli ya kuwanda tembo na nyati  na kwamba hata katika simu zao walikuwa wamehifadhi picha za wanyama hao.









Wednesday, 16 July 2014

RC MORO AKEMEA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDO YA KIJAMII.


 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akifungua mkutano wa 98 wa watayarishaji wa vipindi shirika la utangazaji la Taifa TBC.


Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.



MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera amewataka watumiaji wa mitandao  ya kijamii ,  kuacha tabia ya kutumia mitandao hiyo kwaajili ya kukashfiana , kutoleana lugha chafu na  kudhalilishana na badala yake itumike kwaajili ya kutoa elimu na burudani.


Alisema hayo jana wakati  wa mkutano wa 98 wa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia shirika la Utangazaji Tanzania TBC.


Alisema mitandao hiyo kwa sasa watumiji wamekuwa wakitumia kinyume na malengo, kutokana na kukosa nafasi katika vipindi mbalimbali vya Tv na radio.


‘’ Mara nyingi mashirika ya utangazaji yamekuwa yakitoa nafasi kwa wataalam na viongozi  huku waiwasahau wananchi jambo linalosababisha kutumia mitandao ya kijamii kuweka habari zao’’ alisema


Hata hivyo mkuu huyo aliwataka watoa habari kuacha tabia ya kukwepa kutoa habari kwa waandishi wa habari pale zinapohitajika kwani kufanya hivyo kunasababisha kuandikwa kwa habari zisizo sahihi.


‘’ waandishi wa habari sio watu wa kuwakimbia, wanapohitaji habari wapatie ili waweze kuchuja na kuandika kile kinachofaa’’ Alisema


Hata hivyo aliwataka waandishi wa habari kuacha tabia ya kuandika habari kwa  zenye chuki na kulenga kumdhalilisha mtu bila sababu yeyote.


Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa TBC Clement mshana aliwataka wasemaji wa wizara kujenga tabia ya kuita vyombo vyote vya habari pale wanapotaka kutoa taarifa ya uelimisha umma au zinapofanyika kampeni mbalimbali.


Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha weledi wa utayarishaji wa vipindi mbalimbali katika shirika hilo.


Kwa upande wake  mkurugenzi wa mfuko wa Pensheni wa PSPF Adam Mayingu alisema mfuko huo kwa sasa mfuko huo una wanachama tegemezi wapatao 400,000.


Alisema lengo la kudhamini mafunzo hayo ni kuwafanya watayarishaji hao kuwa na uelewa juu ya  mfuko huo wa PSPF .


WANAOKAIDI KUBOMOA KWA HIARI KATIKA HIFADHI ZA BARABARA KUKUINA CHAMOTO,

 Meya wa Mansipaa ya Morogoro Amiri Nondo akikagua baadhi ya maeneo yaliovunjwa kwaajili ya kupisha ujenzi wa barabara ya Kitope katika manispaa hiyo.

 Meya huyo akizungumza na wananchi katika eneo la Maont Uluguru Hoteli .

 Meya huyo akiangali amaeno ambayo tayari wafanyabiashara walivunja kwa hiari bila shuruti kupisha ujenzi huo wa barabara.

 Meya huyo akiwa katika moja ya barabara zinazotengenezwa  akikagua ujenzi huo.
 Meya Nondo alipofika eneo la jirani na Hotel  Ya Maunti Uluguru akiwaambia wafanyabiashara hao waondoke eneo hilo na ku hamia Fire.

 Meya akizungumza na wajumbe wa kamati ya fedha katika ukumbi wa manispaa ya Morogoro juu ya ziara hiyo.
 meya akiwa katika eneo la hoteli ya Maunti Uluguru ambapo mmiliki wake  hadi sasa hajabomoa kupisha barabara hiyombali na kuwekewa alama nyekundu kama inavyoonekana.

Meya Nondo alipokutana na baba huyo kijana ambaye ameamua kulea mtoto wake wakati mkewe akiwa kazini.

Friday, 11 July 2014

MAMA ATIWA MBARONI KWA KUMFICHA MTOTO WAKE WA MIAKA 5 KILOSA MOROGORO

Polisi mkoani Morogoro inamshikilia mama mmoja   Sara Mazengo kwa tuhuma za kumficha ndani mtoto wake  wa miaka (5) Devita Malole.

 Mama huyo alikamatwa jana katika kijiji cha Matongola Dumila wilayani  Kilosa baada ya viongozi wa kijiji hicho kupata taarifa kuwa kuna mtoto anafichwa na mama huyo.
 hata hivyo mtoto huyo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kwa uchunguzi wa afya huku mama huyo akiwa mbaroni.

Habari zaidi na picha zitawajia badae .


DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO.

Huyo ndiye Karume kauzu Habibu, daktari feki aliyekamatwa  katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akitibu wagonjwa, amekuwa akivaa koti leupe mithiri ya  Daktari. kwa sasa anashikiliwa na polisi.


Amekutwa na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kinaonyesha anarudia mtihani katika kituo kimoja mjini Morogoro, ni mkazi wa Kigoma, kwa sasa alikuwa akiishi Liti manispaa ya Morogoro.

Polisi wanafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

GARI LA MAKAL LAENDELA KUSHIKILIWA NA TRA MORO

     Gari lenye namba za usajiri T  534 BFP Toyota Dyna linalomilikiwa na  Gabriel Amos makal , linaendelea kushikiliwa na mamlaka ya mapato Tanzania mbali na gari hilo kulipiwa deni la sh 662,500 iliokuwa ikidaiwa kama ushuru wa barabara.


Namba ya simu inayodaiwa kutuma ujumbe wa vitisho kwa TRA hiyo hapo.  0763 444455  baada ya gari hilo kukamatwa. 
Ujumbe wa kwanza ''silipi,''
Ujumbe mwingine huu aliotuma ni  ‘’  mazingira ya kukamata hilo gari  ni ya kihuni na ii inaonyesha namna gani ht raia wa kawaida wanavyopata taabu watu hawana vitambulisho, wamewashurutisha  wangu, nabaki na msimamo kuwa zoezi mnalolifanya na kero ninazopokea toka kwa wananchi kuwa TRA Mvomero ni wakatili na wananyanyasa wananchi ss mimi mwakilishi  wa wananchi nimethibitisha, kwa vitendo  najua hatua za kuchukua kny ya wananchi wangu’’ 

TAARIFA ZAIDI ZITAWAJIA HIVI PUNDE.





 

DAWASA KULIPA BILIONI 7.9 WANANCHI WA KIDUNDA MOROGORO KUSINI

 Mkurugenzi wa fedha wa mamlaka ya maji safi na taka Jiji la Dar es Salaam aliyesimama Didas Mwilawi, Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogieris  wapili kushoto kwake, mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi, Mwenyekiti wa halmashauri ya Morogoro Kibena Kingo, na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yona maki ,wakati wa kikao cha watendaji wa  Dawasa na Halmashauri hiyo kutoa maelekezo ya fedha bilioni 7.9 zitakavyoafikia wananchi wanaofidiwa katika bwawa  la Kidunda.

Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakifuatilia  kikao hicho.

Wajumbe walioshirikia kikao hicho ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Bwawa la Kidunda.

Mkurugenzi wa fedha wa Dawasa Mwilawi akitoa ufafanuzi juu ya mgawanyo wa fedha hizo.

Habari zaidi 



JUMLA ya sh Bilioni 7.9 zinatarajiwa kulipwa na Mamlaka ya maji safi  na Taka Jiji la Dar es Salaam   (DAWASA) kwa wananchi wanaoishi karibu na bwawa la Kidunda wilaya ya Morogoro.

Thursday, 3 July 2014

MANISPAA YA MORO YAPOKEA MADAWATI 700 YA FEDHA ZA FIDIA YA RADA.

 Naibu meya wa manispaa ya Morogoro Lidya Mbiaji akikabidhi dawati kwa mkuu wa shule ya msingi Bungo Roman Luoga huku  kaimu afisa elimu wa manispaa ya Morogoro   Christopher Wangwe akishuhudia.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa elimu kata, baada ya kukabidhi madawati ya Plastiki yaliotokana na fidia ya fedha za Rada.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mazimbu B wakifungua maboksi ya madawati hayo .







HALMASHAURI ya  Manispaa ya Morogoro imepokea madawati 756 kutoka Serikali kuu yalionunuliwa kwa fedha za fidia ya Rada.


Madawati hayo aligawiwa jana katika shule 9 za manispaa  hiyo sambamba na vitabu 127,867 vya masomo yanayofundishwa shule za msingi.


Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Lidya Mbiaji alisema hayo jana wakati akikabidhi madawati hayo kwa walimu wakuu wa shule hizo.


Aliwataka wazazi na walezi wa watoto hao kuwajibika katika kuyatunza madawati hayo ili yaweze kudumu na kuondokana na kero ya madawati.


Hata hivyo aliwataka walimu wakuu wa shule zilizopatiwa madawati hayo kuhakikisha wanatoa madawati hayo kwa wanafunzi ambao wenye kuweza kuyatunza .


Kaimu mkurugenzi wa Manispaa hiyo Philemon Magesa alisema madawati hayo yamekuja wakati manispaa hiyo ikiwa na upungufu wa madawati takribani 7000.


 Alisema pamoja na kupata madawati hayo  sio kigezo kwa wazazi na walezi kubweteka katika zoezi la kuchangia suala zima la madawati.


Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Zumo Makame alisema msaada huo utasaidia kuondoa kero kwa wanafunzi ambao walikuwa wakikaa chini kwa kukosa madawati wakati wa kusoma.


Alisema kamati ya huduma za jamii inalenga kuboresha elimu na hivyo kuhakikisha wanaondoa kero zote zinazokabili elimu ili kutoa fulsa kwa wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.