Pages

Subscribe:

Friday, 11 July 2014

DAWASA KULIPA BILIONI 7.9 WANANCHI WA KIDUNDA MOROGORO KUSINI

 Mkurugenzi wa fedha wa mamlaka ya maji safi na taka Jiji la Dar es Salaam aliyesimama Didas Mwilawi, Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogieris  wapili kushoto kwake, mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi, Mwenyekiti wa halmashauri ya Morogoro Kibena Kingo, na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Yona maki ,wakati wa kikao cha watendaji wa  Dawasa na Halmashauri hiyo kutoa maelekezo ya fedha bilioni 7.9 zitakavyoafikia wananchi wanaofidiwa katika bwawa  la Kidunda.

Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakifuatilia  kikao hicho.

Wajumbe walioshirikia kikao hicho ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Bwawa la Kidunda.

Mkurugenzi wa fedha wa Dawasa Mwilawi akitoa ufafanuzi juu ya mgawanyo wa fedha hizo.

Habari zaidi 



JUMLA ya sh Bilioni 7.9 zinatarajiwa kulipwa na Mamlaka ya maji safi  na Taka Jiji la Dar es Salaam   (DAWASA) kwa wananchi wanaoishi karibu na bwawa la Kidunda wilaya ya Morogoro.

Mkurugenzi  wa fedha wa  DAWASA Didas Mwilawi alisema hayo jana wakati wa kikao cha watendaji wa Mamlaka hiyo na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.

Alisema fedha hizo zitalipwa kwa utaratibu wa hundi  kwa wananchi wote ambao  tayari walishahakikiwa na kupewa fomu ya  fidia namba 69.

‘’ Fomu hii ilitolewa na maafisa ardhi wakati wa uthamini wa fidia  na inayo kumbukumbu namba, mfidiwa atatakiwa kuonyesha fomu hiyo kama ushahidi’’ Alisema.

Hata hivyo alisema kwa wananchi walioko jirani na bwawa hilo watatakiwa kuhama ndani ya miezi 6 huku wale wale ambao barabara imepita maeneo yao watatakiwa kuondoka ndani ya miezi mitatu kupisha ujezi  huo.

‘’ Ni lazima tuanze kutengeneza barabara inayoanzia Ngerengere hadi katika bwawa hilo alafu ndipo tuanze ujenzi wa bwawa’’ Alisema.

Mbunge wa jimbo la Morogoro  Kusini Inocent Karogerie aliwataka wananchi hao kuhakikisha fedha hizo wanazitumia kujenga makazi bora na sio kuzitumia katika matumizi mengine.

Mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya Morogoro Kibena Kiongo  aliwataka viongozi kutowalazimisha wananchi hao na kuwachgulia Benk ya kujiunga kwaajili ya zoezi hilo na badala yake wawaache wenyewe wafanye maamuzi.

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Yona Maki alisema tayari viwanja 1000 ( elfu moja vimeshapimwa kwaajili ya  makazi ya wananchi hao.

Alisema watu 2600 ndio wanatakiwa kufidiwa katika zoezi hilo kwa upande wa barabra itakapopita na wale wanaishi jirani na bwawa hilo.

Bwawa la Kidunda linajengwa kwaajili ya kuchukua maji kutoka katika mto Ruvu kwaajili ya   kusaidia kuwa na uhakika wa maji katika kipindi chote cha mwaka.


0 comments:

Post a Comment