Pages

Subscribe:

Thursday, 17 July 2014

MAJAMBAZI SITA WAKAMATWA MORO

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paulo akionyesha moja ya silaha zilizokuwa zikitumika katika matukio ya ujambazi, ni baada ya kukamata majambazi  wanne na kuwatia nguvuni.


Habari zaidi soma hapo chini.



WATU  sita   wanashikiliwa na polisi mkoani hapa , watatu kwa tuhuma za ujambazi na wengine wawili  tuhuma za ujangili.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard Paulo aliwaambia waandishi wa habari  jana ,  kukamatwa ka majambazi na majangili  hao kumetokana na  oparesheni maalumu iliofanywa na jeshi hilo.

Kamanda huyo alisema kuanzia Juni 16 hadi Julai 3 mwaka huu jeshi hilo liliendesha oparesheni hiyo na kufanikikiwa kuwakamata waharifu hao na silaha mbalimbali.

Aliwataja majambzi hao Saidi Salehe (30) mkazi wa Kilosa,  Alayazi Makweya (30) mkazi wa Ludewa na Abdul Mateo maarufu  kama baba Ubaya mkazi wa Turiani Mvomero.

Alisema majambazi hao walikamatwa wakiwa  na bunduki aina ya AK 47 ikiwa na risasi 3  kinyume na sheria.

Hata hivyo kamanda huyo alisema Jeshi hilo pia lilifanikiwa kumtia nguvuni jambazi ambaye tayari aliwahi kufungwa miaka 10 kwa makosa  ya ujambazi.

Kamanda huyo alisema jina la jambazi huyo lime hifadhiwa kwa sababu ya wanaendelea na uchunguzi zaidi na kwamba alikamatwa eneo la Mikumi wilayani Kilosa.

Kamanda huyo alisema Julai 16 mwaka huu jeshi hilo liliwakamata majangili wawili Ayoub Abeid  maarufu  Mkwenejele (36) mkazi wa Kilosa  na Nassoro Mohamed maarufu kwa jina la Kambala.

Kamanda huyo alisema majangili hao walikamatwa katika eneo la Mzombe Tarafa ya Mikumi wilyani Kilosa  baada ya polisi waliokuwa katika oparesheni hiyo kuwatilia mashaka watu hao walikuwa wamevalia makoti makubwa meusi.

Alisema watu hao walikuwa na pikipiki namba T 630 BVH SunLg  na kamba baada ya kuwapekuwa wakuwakuta na silaha aina ya Riffle namba AO48441 na risasi 13   bila kibali cha kumuliki silaha hiyo.

Alisema vitu vingine walivyokutwa navyo majangili hao ni unga na samaki pamoja na mazni wa kupimia bidhaa ambao walikuwa wakiutumia kwa kupima wanyama hao baada ua kuwakamata.

Alisema watuhumiwa hao walipohojiwa walisema wamekuwa wakifanya  shughuli ya kuwanda tembo na nyati  na kwamba hata katika simu zao walikuwa wamehifadhi picha za wanyama hao.









0 comments:

Post a Comment