Pages

Subscribe:

Wednesday, 5 February 2014

WANACHAMA WA CCM KAHAMA WAKATWA MAPANGA BAADA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KATA YA UBAGWE....MH KASULUMBAYI MBUNGE WA MASWA MASHARIKI NA WENGINE WASHIKILIWA NA POLISI KUHUSIKA NA UVAMIZI HUO.


Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro
Wanachama sita wa CCM akiwemo katibu Mwenezi wa chama hicho wilayani Kahama wamejeruhiwa vibaya baada ya kukatwa mapanga na kundi la watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA, katika kata ya Ubagwe Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea jana Majira ya sa moja jioni wakati wafuasi hao wa CCM wakitoka katika mkutano wa Hadhara wa kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Ubagwe wilayani Kahama....
katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa kabisa mkono wake wa kushoto
Waliojeruhuwa katika tukio hilo ni katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na Afisa mtendaji kata ya Ubangwe Alphonce Kimaro ambaye amekatwa panga usoni.
Wengine ni katibu wa umoja wa vijana CCM kata ya Majengo Sebastian Masunga ambaye amekatwa panga kichwani na kukatwa kabisa mkono wake wa kushoto na dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kahama Masoud Melimeli ambaye amekatwa kiganja cha mkono
Pia amejeruhiwa Ramadhani Salumu, ambaye ni muhamasishaji wa chama cha Mapinduzi aliyejeruhiwa mguuni pamoja na Subira Nyangusu, huku ikielezwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo walipasua vioo vya gari la CCM na kuchukua funguo za gari hiyo.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wilaya ya Kahama, Andrew Emanuel majeruhi hao wamelazwa katika hospital ya wilaya hiyo, huku Kimaro, Masunga na Peter ambao hali zao ni mbaya wakipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Dereva wa CCM Wilaya ya Kahama Charles Peter aliyekatwa mapanga Kichwani.
Imedaiwa katika tukio hilo wafuasi hao wa Chadema wamepora fedha zaidi ya shilingi milioni moja na laki tatu kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na simu za mkononi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amesema watuhumiwa 16 wa tukio hilo ambao ni wafuasi wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi, wanashikiliwa na jeshi la polisi Wilaya ya Kahama.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini, IGP Ernest Mangu afanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi nchini



Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi. Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na:
1. Aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara,
2. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.

3. Aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi,

4. Aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na:

5. Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.

Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja;

TASWIRA YA MCHEZO KATI YA SIMBA NA MTIBWA SUGAR KATIKA UWANJA WA JAMUHURI MOROGORO

Kikosi cha Timu ya Soka ya Simba Kilichoanza Dhidi ya Mtibwa leo
Nyuma Kuanzia Kushoto: Kocha Msaidizi Seleman Matola,Tambwe,Amri Kiemba,Joseph Owino,Jonas Mkude,Musoti.Mbele Kushoto:Singano,Awadhi,Haruna Chanongo,Ivo Mapunda,Rashid Baba Ubaya,Haruna Shamte.
 Kikosi cha Timu ya Soka ya Mtibwa Nyuma kuanzia Kushoto:JumaLuizio,Shaban Nditi, Hassan Ramadhan,Ally Shomary  Salim Mbonde.Mbele Kuanzia Kushoto : Jamal Mnyate,Said Mkopi,Shaban Kisiga, Husein Sharif,Salvatory Mtebe,Mussa Mgosi.
Waamuzi wa Mchezo wa Leo wakiwa na Manaodha wa Timu Zote Mbili.
 Wachezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar Wkishanilia Goli Lililofungwa na Musa Mgosi  Katika Dakika ya 18 ya Mchezo.
 Rashid Baba Ubaya Akitafuta Mbinu za Kumtoka Beki wa Mtibwa Sugar Said Mkopi.

UVCCM MORO YAPINGA TAMKO LA MWENYEKITI MKOA MOROGORO, YASEMA NI LAKE BINAFSI, HALINA BARAKA ZA VIKAO, WAENDELEA KUMSISITIZA MALECELA KUOMBA RADHI UVCCM .





 







Ndugu zangu waandishi wa habari

Habari za kazi, na hongereni sana kwa kazi nzuri ya habari mnayoifanya katika jamii yetu.



Ndugu zangu nimewaiteni hapa ili kusema machache na kuendelea kutoa maoni yangu binafsi kama mwanachama hai wa Umoja wa vijana (Uvccm) kuhusu kumsisitiza mzee John Samwel Malecela auombe radhi Umoja wa vijana waTanzania kwa kitendo chake cha kuunga mkono tamko lilitolewa na mkuu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi wa uvccm Tanzania Ndg Paul Makonda,,


Msisitizo wangu unatokana na jinsi gani nilivyosikitishwa na kitendo alichokifanya Mzee Malekela cha kumuunga mkono ndg Makonda,, ambae tamko lake limekataliwa na Mwenyekiti wetu wa Taifa ndg  Sadifa Juma Khamis, kwamba si la umoja wa vijana na si vema kwa wanachama kusemana nje ya vikao, pia makamu mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Tanzania Ndg Mboni Muhita pia amelikataa ya kwamba halitokani na Umoja wa vijana, ikumbukwe kwamba Makamu Mwenyekiti ni mtu wa pili kiitifaki katika umoja wa vijana ukilinganisha na Ndg makonda ambae ni watano katika uvccm. Na ni kiongozi wa idara tu. Mzee malekela kuliunga tamko la Makonda ni kinyume cha utaratibu na amewakosea heshima viongoz wetu wa vijana wa taifa na uvccm yote kwa ujumla.

Mbali na hilo, pia tamko la ndg Makonda limebeba misamiati tata ambayo imesababisha mgongano wa hoja baina ya viongoz wa kiimani na waumini wao wa madhehebu yote ambayo pia ni sehemu ya taifa hili.. mgongano huo wa viongoz wa kiimani na Chama unaweza ukakiathiri Chama chetu kwa kiasi kikubwa.

Ni rahisi sana kwa viongozi wa kiimani kumsamehe ndg Makonda kutoka na rika lake, lakini ni vigumu sana kumuelewa Mzee wa chama kwa kuunga mkono na wanaweza wakahisi kwamba chama kimemtuma ndg Makonda kwenda kuwahusisha katika tamko lake, jambo ambalo sio la kweli. Lkn pia nasikitishwa sana kumuona Mzee wetu huyu kuunga mkono tamko linalomdhalilisha mkt wetu wa vijana taifa na watendaji wake kwa mtu mmoja kuivunja kanuni mbele yao, huku akiudanganya umma kwamba ni tamko la Uvccm..

Ndugu zangu waandishi, naendelea kusisitiza kwamba Mzee Malecela auombe radhi umoja wa vijana Tanzania..

Pamoja na hayo,, pia napenda kutoa maoni yangu binafsi kuhusu maelezo ya mkt wa uvccm mkoa wa Morogoro aliyoyatoa jana kwa waandishi wa habari, yale yalikuwa ni mawazo yake binafsi na sio ya umoja wa vijana kwakuwa hayajapitia katika kikao cha kamati ya utekelezaji cha mkoa,, amefanya vema kuujulisha umma kwamba maoni niliyoyatoa mimi awali yalikuwa ni maoni yangu binafsi na si ya uvccm mkoa kama nayeye pia maoni aliyoyatoa ni yake binafsi na si ya uvccm  mkoa waMorogoro. Na chama kinaruhusu mtu kutoa maoni yake binafsi, nampongeza sana

Lakini pia, si jambo jema kwa kila anayetoa maoni binafsi kuhusu mustakabali wa chama, kuyahusisha maoni yake na maswala ya makundi,, na chama chetu hakijamzuia mwanachama yeyote mmoja mmoja kutoa maoni yake binafsi,, tukianza kuwanyima fursa wanachama kutoa maoni yao kwa mihemko ya makundi, basi tutaikandamiza demokrasia ya ndani ya chama, kama viongoz ni lazima tujue kutofautisha kati ya vichwa vya habari vya habari na habari yenyewe, vinginevyo kutokana na ukubwa wa chama na maoni yanayotolewa na wanachama wa maeneo mbalimbali ya ndani na nje  ya nchi, kutakuwa na watu wa kukanusha au kurekebisha, na wale wa kutoa maoni, CCM ni chama cha wanachama wote,, pasiwepo namna yeyote ile ya kunyimana uhuru.


Naungana na Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Morogoro kumpongeza sana mkt wetu mpendwa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa mkoani Mbea hivi karibuni katika sherehe za kutimiza miaka 37 ya chama chetu imara cha CCM, ni wajibu wetu sote kuyatekeleza yale aliyotuagiza mhe mkt wetu wa CCM taifa. Na hasa kuheshimu maamuzi yatokanayo na vikao


Ndg zangu mkoa wa Morogoro umekumbwa na matatizo mengi sana, ikiwa pamoja na mapigano ya wakulima na wafugaji, na mafuriko yaliyotokea wilayani kilosa na mvomero,, nami napenda kutoa pole kwa wahanga wa matatizo hayo, na kuunga mkono maoni ya mkt wa uvccm mkoa kwa wadau mabalimbali kujitokeza katika kusaidia wahanga, pia nawapongeza sana viongozi wa serikali na chama wote kwa kuwajibika kutatua na kusaidia katika swala hili..

Lakini ni vema sana kwa sisi vijana kuwa wa kwanza na mstari wa mbele kufika katika maeneo ya matukio mapema ili kuona hali na kushiriki katika hatua za awali,, tusijifunze kutoa pole kwenye vyombo vya habari baada ya matukio kuwa yameshapita na hatujafika hata eneo lenyewe la tukio.. hapo tutakuwa tunaonekana tunafanya siasa badala ya kazi.. lakini kutoa maelekezo au wito katika maeneo ya majanga ambayo tayari mkt wetu wa taifa ameshafika na kufanya hivyo, ni makosa ambayo tunahitajika kujifunza…

Napenda sana kutoa pongez zangu binafsi kwa vijana wa uvccm wilaya ya mjini na wale wa kilosa kwa jinsi wanavyoshiriki kikamilifu katika shughuli za kampeni katika katika chaguz za marudio kata ya tungi na ludewa, ni maoni yangu binafsi kwamba na sisi wanachama wengine tushiriki kikamilifu, badala ya kutoa maoni huku tukiwa hatujawahi hata kufika katika eneo la tukio. Hasa katika maeneo amabayo kuna chaguzi za marudio ndani ya taifa letu

Pia ni maoni yangu kwa vyama siasa hususani chadema kuacha kampeni za vurugu na kujeruhiana ambazo zinawadhuru wananchi, kuwanyima amani na kuzorotesha shughuli zao za kiuchumi, tufanye kempeni za kiistarabu, za hoja na amani kama ilivyo desturi ya nchi yetu, pia vyombo vya ulinzi naviomba viongeze umakini zadi katika kipindi hiki hasa katika maeneo yale ambayo kampeni zinafanyika..

Asanteni kwa kunisikiliza, nawatakia kazi njema!!

IMETOLEWA NA

HERI HOZA
Mjumbe wa kamati yautekelezaji ya baraza la UVCCM
Mkoa wa Morogoro





Tuesday, 4 February 2014

ANGALIA TASWIRA YA MECHI YA KIRAFIKI KATI YA MORO VETERAN NA TANGA VETERAN

 Manaodha wa Timu ya Moro Vetrani na Tnga Veteran  Wakiwa na Waamuzi wa Mchezo huo Uliofanyika Morogoro. 
Timu hicho zilicheza Mchezo wa Kirafiki Katika Uwanja wa Mochwari mKoani Morogoro Mara daaba ya Timu ya Tanga Veterani Kufanya ziara ya Kudumisha Urafiki na Undugu walionao dhidi ya Timu ya Morogoto Vetrani.Katika Mchezo Huo Wenyeji Timu ya Morogoro Veterani Walishinda kwa Jumla ya Magoli 2 kwa Moja.Magoli ya Moro Veterani Yalifungwa na Mokili Rambo dk 35 na 72 Wakati Goli la kufutia Machozi la Tnga Veterani Lilifungwa Dk 80.
Kikosi cha  Timu ya Tanga Veterani Kilichoanza katika Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya Morogoro Veteran
Wenyeji wa Mchezo huo Timu ya Morogoro Veterani wakiwa katika picha ya pamoja.
Mashabiki waliojitokeza katika Mchezo huo
Mchezaji wa Morogoro Veterani Boniface Mapunda akiwa na Mpira sambamba na Mchezaji wa zamani wa Timu za Ligi kuu za Moro united,Ynaga na Ruvu Shooting Benjami Haule
Mchezajiwa zamani wa timu ya Polisi Morogo Juma Khamisi akiwa na Mpira wakati wa Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya Timu ya Tanga Veterani
Moja ya Purukushani katika mchezo huo katika Lango la Timu ya Tanga Veterani



Wachezaji wa Timu ya Morogoro Veterani wakimpongeza Mcheazji Wa zamani wa Polisi Morogoro Mokil Rambo mara baada ya kuwafungia Goli la Kuuongoza.

UVCCM MORO YAKANUSHA MATAMKO YANAYOTOLEWA HOVYOHOVYO, YASEMA NI MATAMKO YAO BINAFSI NA SI YA UVCCM .

 Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Morogoro Harriet Sutta akiwa na katibu wake Nicodemas Tambo wakizungumiza juu matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi mkoani hapa kinyume na taratibu.
Mimi nazungumzia juu ya uchaguzi tulionao mbele yetu katika wilaya ya Gairo ludewa na Tungi Manispaa ya Morogoro, vijana washiriki kikamilifu kufanya kampeni za amani na utulivi na sio vurugu.

Kwa habari zaidi, soma hapa chini.




TAARIFA YA UVCCM MKOA WA MOROGORO KWA WAANDISHI WA HABARI.



Ndugu zangu waandishi wa habari Mliokusanyika Hapa ….
Kaka zangu na dada zangu asalamu alekum….
Tumsifu yesu kristo……………
Awali ya yote, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema kwa kutukutanisha pamoja katika siku hii ya leo ili tupate kuongea machache yanayoendelea katika Taifa letu na husani katika chama chetu cha Mapinduzi CCM. Lakini Pia niwashukuru sana kwa kukubali kuitikia wito wangu na kufika mahala hapa kwa wakati na kwa mda muafaka Nawashukuruni sana, Na nawasahii muendelee na Moyo huo huo, mara zote mkihitajika sehemu yoyote ile, Maana ninyi ni nguzo Muhimu saana katika kuupa uma wa watanzania taarifa mbalimbali zinazoendelea katika Taifa lao.
Baada ya kusema hayo sina Budi kuwaelezeni sasa kwa nini Nimekuiteni hapa, Siku chache zilizopita mnamo Tarehe 2/02/2014 chama cha mapinduzi kiliazimisha Miaka 37 ya kuzaliwa kwake, sherehe hizo zilifanyika katika Mkoa wa Mbeya  na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa  na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa Naiba Ya jumuiya ya Vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro  (UVCCM ) ninachukua Nafasi hii Kumpokeza Mweshimiwa Dr. Jakaya Kikwete Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa Hotuba yake nzuri alioitoa katika kilele hicho cha maadhimisho ya sherehe hizo za kuzaliwa kwa CCM. Lakini pia Kwa niaba ya UVCCM mkoa wa morogoro ninaomba yale yote alioyoyagiza Yatekelezwe Haraka kwani ninaamini yatafufua uhai wa chama na Kukiimarisha zaidi lakini pia kukiletea chama cha Mapinduzi Ushindi endapo yatatekelezwa  kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Ndugu zangu waandishi wa habari, Lakini pia nichukue nafasi hii kurekebisha baadhi ya mambo yaliojitokeza katika Mkoa  wetu wa Morogoro Hasa katika Jumuiya yetu ya  Vijana. Kumekumekuwepo na Matamko mbalimbali yaliotolewa na baadhi ya  viongozi wa jumuiya  Yakihusishwa na Umoja wa Vijana Mkoa wa Morogoro. Naomba ifahamike kua uvccm ni taasisi ambayo ina miongozo na mfumo rasmi wa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku.  Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za umoja wa vijana Msemaji wa Jumiya ya Vijana mkoa wa Morogoro Ni mwenyekiti wa UVCCM MKOA au Katibu Wa UVCCM Mkoa kama italazimika Mtu mwingine kusema basi ni kwa idhini maalumu ya Mwenyekiti
Wahenga walisema “kila panapotokea  kosa lolote lile  kuna jambo  la kujifunza” hivyo hakuna kosa lisilo na faida  Kupitia haya yaliotokea katika Mkoa wetu naomba pia iwe Fundisho kwenu waandishi  habari kila mkiitwa na Mtu yoyote anaetaka kuongea nanyi kama anaongea nanyi kwa niaba ya Tasisi ni vema mkafwatalia na mkajiridhisha kama ni Msemaji sahihi wa Tasisi Hiyo ili Kuepuka malumbano yasio na Tija
Kabla sijamaliza ningeomba pia kuchukua Fursa hii kuwapatia pole wakazi wa wilaya ya Kilosa kwa mafuriko yaliowapata ninaamini wapo katika wakati Mgumu hasa baada ya kuharibiwa makazi yao, na kuharibiwa mali zao. Nichukue nafasi hii kuwatia Moyo na kuwahakikishia serikali ya Chama cha Mapinduzi itahakikisha wanapatiwa stahiki zote anazotakiwa mtu kupewa na serikali yake yanapotokea majanga kama hayo.
Lakini pia niyaombe mashirika yasio ya kiserikali mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wenye uwezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kuwafariji wana kilosa waliopatwa na mafuriko hayo na kuwaapa misaada ya kila namna inayostahili.
Mwisho ninaomba Kampeni zinazoendelea katika Mkoa wetu kata ya Tungi na Rudewa zifanyike kwa amani na ninawaomba vijana wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo mdogo kua wastaarabu na waadilifu wajivunie kulinda misingi ya Taifa hili amani upendo na mshikamano uchaguzi usiwagawe na kueneza chuki baina yao hivyo ninawasihi washiriki kampeni hizo kwa amani na utulivu “wakubali kutofautiana kisera na kwa hoja ” ila “wasikubali kufarakana” Vijana tunahitaji Uvumilivu wa kisiasa ili tukomae katika siasa na Demokrasia ya kweli
Niwashukuru saana kwa Kunisikiliza…..
Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na Harriet Sutta
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA
MOROGORO
04/01/2014

Monday, 3 February 2014

KIMENUKA TUNGI, WAFUASI WA CHEDEMA WAWATWANGA CCM, MMOJA AJERUHIWA NA KULAZWA

 Kada wa umoja wa Vijana mkoa wa Morogoro Daniel Richard aliyelazwa wodi namba moja katika hospitali ya mkoa wa Morogoro baada ya Chadema kuwavamia na kuanza kuwapiga wakati wakitoka katika kampeni ndogo za udiwani kata ya tungi Manispaa ya Morogoro.
 Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Lomuli akijadili jambo na viongozi wa CCM wilaya ya Morogoro mjini nje ya wodi namba moja walikokwenda kumwona kada huyo.

 Huyu ni miongoni mwa vijana 80 wanaodaiwa kuletwa manispaa ya Morogoro kwaajili ya kufanya vurugu wakati wa kampeni za uchaguzi  wa udiwani tungi, alikamatwa baaada ya kumpiga mmoja wa makada mjini hapa ambaye amelazwa Hopitali ya mkoa,

 Hii ni pikipiki aliyokmatwa nayo kijana huyo wa Chadema wakati wa vurugu hizo akiwa chini ya ulinzi wa polisi

 Hii ni pikipiki aliokamatwa nayo mfuasi huyo wa Chadema ikiwa na nambo ya chama hicho.
 Pikipiki hiyo ikiwa ndani ya gari la polisi

Wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro wakimjulia hali kada huyo.