Pages

Subscribe:

Thursday, 23 January 2014

WAZIRI MKUU ATEMBELEA WAHANGA WA MAFURIKO DUMILA, AWAHAKIKISHIA UHAKIKA WA CHAKULA NA DAWA

 
 

Wednesday, 22 January 2014

MAFURIKO MAKUBWA DUMILA, DARAJA LAKATIKA, HAKUNA MAWASILIANO DODOMA NA MOROGORO

BREAKING NEWS; 

Maafa makubwa yametokea eneo la Dumila wilayani Kilosa na eneo la Dakawa wilayani Mvomero, kutokana na mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Kilosa na kusababisha daraja la Dumila katika barabara kuu ya Dodoma na Morogoro kukatika.

Kwa sasa hali si shwari magari yanashindwa kupita na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayotoka Dodoma kwenda Dar , na yanayotoka Dar kwenda Dodoma.

Taarifa zaidi tutawaletea punde.

ZIARA YA KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YA MANISPAA YA MOROGORO



 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akipata maelezo kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya ujirani iliopo kata ya Kihonda Philemon Kibuja wakati wa ziara ya kamati ya fedha ya manispaa hiyo.


 Tumeleta milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hii, ili wanafunzi wetu waweze kusoma vizuri. Amiri Nondo akiongea katika ziara hiyo.




 Wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani wakiwa katika moja ya chumba cha madarsa katika shule hiyo.


 Tumeleta milioni 600 katika Hospitali ya wilaya inayojengwa hapa Kiegea ili kurahisisha huduma ya afya kwa wakazi wa huku na jirani. meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akitoa taarifa kwa kamati hiyo.



 Meya huyo akiangalia moja ya nguzo inayojengwa katika Hospitali hiyo ya wilaya ya manispaa ya Morogoro.


 Madiwani na watendaji wa manispaa ya Morogoro wakiongea na injinia wa kampuni ya Mzinga inayofanya ujenzi katika hospitali hiyo ya wilaya.


 Kwa kawaida ujenzi wa kampuni ya mzinga tunaukubali, ni maneno ya Maya Nondo.


 Baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo cha afya cha Uhuru maarufu kama Nunge .


 Diwani wa kata ya Kingo Fidelis tailo akimpa maelezo meya wa manispaa ya Morogoro kuwa hospitali hiyo imeelemewa, . hakuna stoo, madaktari wanatumia chumba kimoja wanne, huduma za usiri kwa wagonjwa hakuna.


 Nimechelewa kidogo maana ratiba sikuipata vizuri, karibuni jamani Mjimpya, ni diwani wa Mjimpya Wensilaus akiwakaribisha madiwani wenzake waliotembelea stendi mpya ya magari yanayokwenda nje ya manispaa ya Morogoro.


Hapa ndio yatapakia magari ya Mgeta, stendi hii itapunguza msongamano pale mjini .


Tuesday, 21 January 2014

Uzinduzi wa kampeni za udiwani Ludewa

 Mapokezi ya makada wa CCM katika uzinduzi wa kampeni ya udiwani katika kata ya Ludewa wilayani Kilosa

 Haya niambieni mambo yamekaaje, leo ndio tunazindua lazima tujue ushindi ni lazima kwa CCM , ni maneno yake katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Lomuli

 Hadi kieleweke, si unajua tena shughili bila Kwaito haijafana

 Chonde chonde wanaCCM kura zenu kwa Subiri Joseph apate udiwani kata ya Ludewa jamani, shuka kwa shuka, kitanda kwa kitanda hadi kieleweke, Mariamu Kiamani akiweka asili yake ya wahehe, bila goti hakijaeleweka.



Ndugu zangu wa Ludewa kura zote kwa CCM sawa eheeee, Juliana Mwenda akimwaga sera zake jukwaani.

 CCM ndio chama pekee kinachoweza kuitawala Tanzania, jamani naomba tusipoteze kura, ili tupate maendeleo ni lazima tuchague CCM. maneno ya Romuli.

 Mwaka wako ni mmoja kama hujafanya kitu ujue safari ijayo OUT, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Inocent Karogeries akimwambia  mgombea udiwani wakati wa kampeni za kumnadi.

Mmemuona huyo, si tunafanana naye, naomba mumpe kura nifanye naye kazi. Mwenyekiti wa CCm wilaya ya Kilosa Udelele akiwaambia wananchi wa Ludewa.

Wednesday, 15 January 2014

CCM MORO MJINI YAWATAKA WALIOGOMBEA UDIWANI TUNGI KUUNGA MKONO ALIYETEULIWA .


 Mgombea udiwani kata ya Tungi manispaa ya Morogoro kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Deogratias Mzeru akikabidhi fomu ya kuwania udiwani kwa mtendaji wa kata hiyo Abuu Liwangira Januari 15 mwaka huu.
 Mgombea Udiwani Mzeru akikabidhi fomu zake kwa mtendaji wa kata ya Tungi mbela ya katibu wa CCm wilaya ya morogoro mjini Ali Isa.
 Hongera Mzeru, tumekuja kukuunga mkono wenzako, ni wagombea udiwani wa kata ya Tungi Lusajo Manase na Godfrey Taiko .
 Tuko pamoja na ushindi ni lazima, mimi niko CCM muda mrefu sana hivyo lazima tuhakikishe CCM inashinda Tungi. Godfrey Taiko akimwambia mgombe mwenzake Mzeru waliomsindikiza kuchukua fomu ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho.
 Pamoja sana Mzeru, tumekuja kukusindikiza , CCM ushindi ni lazima.
 katibu kata  wa CCM kata ya Tungi Zulfa akiwa katika picha ya pamoja na wagombea udiwani wa kata hiyo.
 Nani kasema imekaa vibaya, CCM imekaa vizuri, . Mzeru amekaa vizuri. jeshi la CCM ndani ya Tungi.
 Mnajua sisi wanawake lazima tuhakikishe kinaeleweka hapa Tungi ama sivyo jamani, katibu wa UWT Dotto akiwaambia wanawake wa manispaa ya Morogoro
 Vijana wa CCM wakia nje ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Tungi wakisubiri mgombea udiwani Mzeru kurejesha fomu.
 Hatutaki matusi, wala kejeri katika uchaguzi huu, kila chama kinadi sera zake, wananchi wanahitaji sera na maendeleo na sio matusi, Mgombea udiwani kata ya Tungi kwa tiketi ya chama cha Jahazi Asilia Ismail Ismail . alipofika katika ofisi ya kata na kuongea na wanachama wa CCM.
 Makada wa CCM wakijadiliana nje ya ofisi ya mtendaji kata ya Tungi
 Viongozi wa CCM wilaya ya Morogoro mjini wakisubiri mgombea wao Mzeru kurejesha fomu nje ya ofisi ya mtendaji kata ya Tungi.
Wananchi wa kata ya Tungi waliomsindikiza mgombea wao Mzeru kurejesha fomu wakiwa katika picha ya pamoja.



CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro kimewataka wagombea udiwani katika kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro ambao hawakuteuliwa kushirikiana na mgombea aliyeteuliwa katika kukupatia ushindi wa kishindo.
Katibu wa CCm wilaya hiyo Ali Isa alisema hayo jana wakati akiongea na baadhi ya wagombea hao katika kata ya Tungi mara baada ya Mgombe udiwani aliyeteuliwa na CCM Deogratias Mzeru kurejesha fomu katika ofisi ya mtendaji kata wa Tungi.
Alisema kuwa CCm inautaratibu katika mchakato wa kupata viongozi na kwamba katika mchakato huo wagombea ambao hawakuteuliwa wasikate tamaa.
Alisema kuwa CCM itaanza mikutano yake ya ndani Januari 16 mwaka hu na kwamba wanatarajia kuzindia kampeni rasmi januari 26 mwaka huu ambapo mgeni Rasmi atakuwa Asha Rose Migiro ambaye ndio mlezi wa wilaya hiyo.
‘’ wagombea ambao hawakupata fulsa ya kuteuliwa nawaomba washirikiane katika kumnadi huyo aliyeteuliwa ili CCM ishinde kwa kishindo’’ Alisema.
Kwa upande wao wagombea hao Godfrey Taiko alisema kuwa yeye ni kada wa siku nyingi ndani ya CCm na kwamba kutoteuliwa katika nafasi hiyo hakuwezi kumfanya akakisaliti chama na kwamba nafasi ziko nyingi anaimani atapata nafasi zingine.
Naye Lusajo Mwambogo alisema kuwa atashirikiana vizuri katika kumnadi mgombe huyo ili kuhakikisha CCm inashinda kwa lengo la kuletea maendeleo kata hiyo ya Tungi.
Uchaguzi huo umekuja baada ya diwani wa kata hiyo Daud Mbao kufariki dunia kutokana na kuugua kwa muda mrefu Ugonjwa wa Kisukari.


Monday, 13 January 2014

MZERU AULA UDIWANI TUNGI MANISPAA YA MOROGORO


 Huyu ndiye  Deogratias Mzeru , mgombea udiwani mteule wa chama cha mapinduzi CCM katika kata ya Tungi manispaa ya Morogoro, ameteuliwa  Januari 13 mwaka huu. baada ya kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro kuketi.
 Safari ya kwenda Tungi ilivyoanza, ilikuwa ni safari ya kwenda kumsindikiza mgombea udiwani mteule wa kata hiyo kuchukua fomu ya serikali ili kuingia katika kinyang'anyiro hicho.
 Hapo wazee wa kata ya Tungi wakimsindikiza kijana wao Mzeru kwenda kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika ngazi ya serikali.
 Ni katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Tungi, Mzeru akiangalia kwa makini fomu alizopewa kwaajili ya kuomba ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.
 Wiii, waaaaa, vijana wangu wote mmeenea, sasa tuanze mchakamchaka, ni maneno ya mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Morogoro Salamu Mkolwe wakati za zoezi la kuchukua fomu kwa mgombea udiwani wa kata ya Tungi.
 Tunashukuru sana afisa mtendaji wetu, acha sasa tukajaze fomu hii, tuterejesha kesho mapemaaaa.
 CCM ahaaaa, CCM inawenyewe, chezea CCM weye, haaaahaaa, ni maneno ya makada mashuhuri manispaa ya Morogoro yaliokuwa yakisikika wakati wa ndremo hiyo katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Tungi.
 CCM ninavyoipenda nitakunywa sumu juu yake, makada wa CCM wakiserebuka .
 Siami chama weee, siamii, na mzeru yupo weee, siami, makada wakiimba wakifurahia wakati wa diwani mteule mzeru akichukua fomu ya serikali kuwania udiwani kata ya Tungi.
 Mgombea Udiwani wa kata ya Tungi Mzeru, katibu wa UWT Dotto na katibu wa CCM wilaya Ali Isa  wakiteta jambo na mgombe huyo.
 Tumekuja manispaa kukamilisha taratibu zingine za kiutumishi.
 Mgombea udiwani Mzeru akiwa katika taratibu za kukamilisha mambo fulani ya kiutendaji.
 Mke wangu, umekuja kuniunga mkono mama, asante mwaya, nimeshachukua fomu tayari ngoja nikajaze, si unajua muda wenyewe uliobakia mdogo. 
 Sisi kwa pamoja tunakuunga mkono, tunakutakia kila la kheri. ni wananchi wa kata ya Tungi wakiwa katika picha ya pamoja na mgombea udiwani wao.
 Kila cheleko ina mwenye, wazee wa kata ya Tungi wakimsindikiza kijana wao mara baada ya kuchukua fomu.
 Ni mimi jamani Mzeru wa CCM, naomba ushirikiano wenu, kwa pamoja tutashinda.