Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika eneo la Dumila wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwaajili ya kuwatembelea wahanga wa mafuriko na kujionea hali halisi.
Rais Kikwete akitembela maeneo mbalimbali yaliokubwa na mafuriko hayo.
Rais Kikwete akiwa katika daraja la Mto mkundi lilopo Dumila Kilosa ambalo lilikatika kutokana na mafuriko.
Nilazima tuangalie jinsi gani ya kufanya ili kuzuia mafuriko haya yasiwe na athari kubwa kama hizi. Kikwete akitoa malekezo kwa viongozi wa mkoa na wilaya za Gairo, Kilosa na Mvomero ambazo zimekubwa na mafuriko hayo.
Mheshimiwa mimi ni muhaisis wa chama miaka dahali sasa, nimekubwa na mafuriko kila kitu changu kimesombwa hadi kadi yangu ya chama, Salma Matewele akimwambia Kikwete.
jamani poleni sana na mafuriko yaliowakubwa, kikwete akiwaambia wahanga wa mafuriko hayo katika eneo la Magole ambako ndiko walipoweka katika kambi.
Mheshimiwa hapa tuna kontena tatu za dawa, hakunatatizo kabisa, mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Mtei akimwambia kikwete.
Wananchi waliofurika katika eneo la Mateteni kwaajili ya kumsikiliza kikwete kufutia mafuriko hayo.
katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akiwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilosa nasoro Udelele
RAIS Jakaya Kikwete amewabana wakurugenzi wa halmahsuri na wakuu wa wilaya za Kilosa, Mvomero
na Gairo kuandaa taarifa sahihi ya wananchi walioathirika na mafuriko kwa idadi sahihi sambamba na majina ya wananchi hao na kutaka apatiwe taarifa hiyo kesho mapema.
Rais Kikwete alisema hayo Janauri 27 mwaka huu wakati
alipotembela katika eneo la Magole wilayani
Kilosa kuwapa pole wahanga hao na kujionea hali halisi ya mafuriko hayo.
Kikwete alisema kuwa kutokuwa na takwimu sahihi na majina ya watu hao
kutasababisha misaada hiyo kuwafikia watu ambao hawajaathirika na hivyo
kushindwa kuwafikia wahanga halisi.
‘’ Ni lazima
mjiridhishe kwa kuwatambua watu kwa
majina na jinsia zao, hivi nikisema sasa hivi mkanionyeshe hao watu wapo’’
Alihoji Rais.
Alisema amelazimika kusema hayo baada ya mkuu wa mkoa wa
Morogoro Joel Bendara kusoma taarifa ya
maafa hayo kuwa hadi sasa wananchi wapatao 12472 hawana makazi ya kuishi kutokana
na mafuriko huku akidai kuwa , idadi ya kaya
zilizoathirika 2759,nyumba zilizozungukwa na maji 2922 na nyumba zilizobomoka
ni 1141.
Alisema kuwa kutokuwa
na majina hayo kunamtia mashaka yeye kuwa takwimu hizo huenda sio sahihi
jambo lililomfanya kuwataka kuhakiki upya na kutoa taarifa hiyo ifikapo Kesho.
‘’Uongozi unapimwa wakati wa matatizo, kutokuwa na majina na
idadi sahihi kunaonyesha jinsi gani
msivyowajibika katika kutekeleza majukumu yenu’’ alisema.
Alisema kuwa wakati
wa mafuriko kama hayo yaliotokea mwaka 2009 wilayani Kilosa Mkuu wa wilaya wa
wakati huo Halima Dendegu aliweza kufanya vizuri kwa kuwa na idadi sahihi na kamili.
‘’ Halima alifanya vizuri wakati ule japo alikuwa mwanamke, nyie hapa wanaume
mnashindwa , wakati ule Halima alisimamia vizuri mkaanza maneno yenu ya hovyo,
mlimsema kwakuwa alikuwa mkali,, Alisema
Hata hivyo Kikwete aliwataka wenye viwanda vya magodoro hapa
nchini wanawapatia magodoro hayo ili yaweze kutumika kwa wahanga hao na kwamba
hata kama hakuna fedha watalipwa badae.
Alisema kuwa chakula kipo cha kutosha na kwamba hakuna
mwananchi ambaye atakufa kwa njaa na lengo la serikali ni kuhakikisha kila
mwananchi anapata hudmua muhimu kama chakula, malazi na dawa pamoja na maji
safi.
Alisema kuwa serikali itahakikisha huduma hizo zote
zinapatikana kwa kipindi chote hiki ili
kuokoa maisha ya wananchi hao.
Alisema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa mganga mku wa mkoa
wa Morogoro kuwa hadi sasa wametibiwa wananchi 300 na kwamba magonjwa
yanayosumbua ni kichomi na nimonia ambayo yanasabishwa na kulala chini jambo
ambalo tayari ameagiza kila mwananchi kupatiwa gororo ili kuepuka magonjwa
hayo.
Pia aliagiza uongozi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro
kuhakikisha wanatoa magogo na miti ilioziba katika mito na mifereji ili kuepuka
maafa kama hayo katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendela kunyesha.
Alisema kuwa mafuriko kama hayo sio mara ya kwanza kutokea
kwa wilaya ya kilosa hivyo ni lazima wananchi na serikali kwa ujumla ikachukua
tahadhari ili kuepuka maafa kama hayo
kutokea.
Kwa upande mwingine Rais huyo alisema kuwa atayatumia
majeshi ya hapa nchini katika ujenzi wa nyumba za muda badala ya kuzitumia
halmashauri ambazo zimekuwa na milolongo mingi
ambayo itatoa mianya ya wizi wa vifaa hivyo vya waathirika.
‘’ Ukizitumia halmashauri
waanze kutangaza zabuni, hapo bado watu hawajafikiria kila mtu atapata nini, hakuna
kitakachofanyika, wanajeshi hao tuliwatumia
hata katika mafuriko ya 2009 yaliotokea Kilosa na walifanya vizuri na
sasa tutawatumia tena alisema.
Awali mkuu wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa tayari
walishanza kupokea misaada mbalimbali ikiwamo ya milioni 50,000 kutoka ofisi ya waziri mkuu,
milioni 10,000 kutoka Islamic Foundationi sambamba na dawa za milioni 80,000 kwaajili ya magonjwa mbalimbali.