Pages

Subscribe:

Friday 7 February 2014

MANGULA ASEMA MITANDAO YOTE YA KAMPENI ZA URAIS WAMESHAIBAINI WATAISHUGHULIKIA

 Makamo mwenyekiti wa CCm Taifa Philipo Mangula akivishwa skafu na chipukizi baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Morogoro.

 Makamo mwenyekiti huyo akisalimiana na mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro Juliana Mwenda.
makamo huyo akisalimiana na katibu wa UVCCM mkoa wa Morogoro Nicodemas.
 Makamo huyo akiongea na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro pamoja na wa wilaya ya Morogoro mjini.

Hayo ni mapokezi aliopata alipoingia  katika kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa

Mangula akifungua shina la wakereketwa la Njia panda katika kata hiyo ya Rudewa
 Maelfu waliofurika katika kata hiyo wakati wa kampeni ya udiwani ya Rudewa.
 Mangula akiwa na mgombea wa udiwani kata ya Rudewa Subiri Joseph.

Habari zaidi soma hapa chini.

MAKAMO Mwenyekiti  wa chama cha Mapinduzi Taifa Philipo Mangula amesema kuwa muda wa kampeni  za Urais,udiwani, ubunge na hata nafasi za serikali za mitaa bado   na kwamba wanaofanya kampeni wanakiuka katiba na kanuni na hivyo  CCM inatambua mitandao yote na itawashughulikia.
Alisema hayo Februari 8 mwaka huu wakati akiongea na viongozi wa wilaya na mkoa wa Morogoro alipofika kwajili ya kampeni  za Uchaguzi mdogo  wa udiwani katika kata za Ludewa wilayani Kilosa na Tungi Manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa tayari walishafungua mafaili ya watu hao wenye mitandao ya kampeni na kwamba wanatambua mitandao yote hata katika ngazi za mikoa na watawashughulikia.
Alisema kuwa Rais, wabunge na madiwani waliopo madarakani   bajeti yao ya mwisho  inashia mwezi Juni 2015  na kwamba wanaojitokeza sasa ni waharifu na lazima wachukuliwe hatua.
 Aidha alisema kuwa Viongozi waliopo madarakani wanahaki zote na kwamba ni lazima walindwe ili waweze kufanya kazi zao vizuri bila kunyanyasika na kwamba kuanza kampeni hizo kunafanya kuwavunja nguvu viongozi hao.
‘’Mara zote tatizo la kuanzisha makundi kabla ya kampeni ni kusababisha chuki na uhasama na kupelekea makundi hayo kurushiana maneno, na hiyo inasababisha hata nchi kushindwa kutaalika’’ Alisema
Aliwataka viongozi kutengeneza mitandao ya kuwafutilia watu hao wenyekufanya kampeni za chini kwa chini kinyume na taratibu na kukabiliana nazo .
‘’ Ni mwiko kwa mtu kuunda vikundi na kufanya kampeni za chini kwa chini , tutakabiliana nazo’’ alisema.
Alisema kuwa suala la kutangaza nia ya kutaka kugombea nafasi yeyote sio kosa bali kuanza kampeni ndio kosa kubwa kimaadili ya chama.
Kwa upande mwingine Mangula alisema kuwa wabunge na madiwani kufanya zaira za mara kwa mara ni sawa na mkulima kupalilia shamba lake hivyo wanaodharau kufanya hivyo wasije kulaumu na kwamba watavuna walichopanda.
‘’ Ni dhambi kubwa  kwa mbunge kutotekeleza ahadi  zake, ni sawa na mkulima kupanda mbegu pasipo kufanya palizi, akikuta mazao yake yameliwa na magugu atamlaumu nani’’ Alisema.
Kwa upande mwingne Mangula alisema kuwa nia ya mwenyekiti wa CCm taifa Rais jakaya Kikwete ni kuhakikisha katiba inakamilika haraka  ili itumike katika uchaguzi ujao.
Alisema kuwa itakuwa vema ndani ya siku 70 zilizopangwa kwaajili ya bunge la katiba ikakamilika na kurejeshwa kwa wananchi  ili kutimiza malengo yaliokusudiwa.
Awali katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi walionuna baada ya majina walioyataka kurejeshwa katika uchaguzi huo kutorudi na hivyo kususia kampeni  jambo ambalo Mangula alisema kuwa si dhambi kurejeshwa kwa mgombe wa nafasi ya 3 kinachozingatiwa ni vigezo.
Pia alisema kuwa katika kata ya Ludewa wananchi wake wanalalamikia mbunge wao Mustapha Mkulo kutotimiza ahadi alizoahidi.




0 comments:

Post a Comment