UVCCM MORO YAMTOLEA UVIVU MALECELA
Kutokana
na malumbano yanayoendelea kati ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi hususani
Jumuiya ya Umoja wa vijana (UVCCM) kutokana na matamko yanayoendelea kutolewa.
Ni
jambo la kushangaza sana kumuona Mzee Mashuhuri na nguli wa Chama cha Mapinduzi
Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu kumuunga mkono kijana
aliyekiuka katiba ya Chama cha Mapinduzi na kanuni za Umoja wa Vijana Paul
Makonda kutokana na kauli yake ya kuudanganya Umma kuwa tamko alilolitoa la
kumkashifu Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa NEC ndugu Edward Lowassa kuwa ni la
Umoja wa Vijana. Vifungu vilivyo kiukwa kikanuni na kikatiba ni vifuatavyo:-
Makonda
amekiuka katiba ya CCM Ibara ya 14(4) Mwanachama yeyote atakuwa na haki
zifuatazo “Haki ya kujitetea au kutoa maelezo mbele ya kikao cha CCM
kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake. Pamoja na haki ya
kukata ya kwenda katika kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo
hakuridhika na hukumu iliyotolewa”
Kwa
kuwa kifungu hiki kinatoa fulsa kwa Mwanachama kujitetea juu ya tuhuma
zinazomkabili.
Je
Chama cha Mapinduzi kiliwahi kumuita Mh. Edward Lowassa na wengineo wote wenye
kashfa za rushwa na kutangaza nia ya Urais kumhoji na kumsikiliza na Chama
kufanya maamuzi? Lakini kutoa matamko kupitia kofia ya Chama ni makosa makubwa
yaliyofanywa na Makonda na anapaswa awajibishwe. Tunamshangaa pia Mzee Malecela
kuunga mkono mtu aliyekiuka haki za mwanachama na utaratibu wa Chama. Huu ni
ukweli kuwa tegemeo la Wazee wa CCM kusimamia haki na wajibu wa Chama
umetoweka.
Lakini
pia Mzee Malecela anamtuhumu Edward Lowassa kuchangia harambee, kugawa tisheti
na kutoa misaada katika nyumba za Ibada Kanisani na Misikitini. Mbona wapo
wanachama wengi wanaofanya harambee kama hizo mfano ni Benard Membe, Sumaye,
Samwel Sitta na January Makamba wao pia wanatenda matendo ayatendayo Lowassa
mbona hawajatolewa matamko. Wametengeneza hadi na kalenda kama sehemu ya
kujinadi mwaka 2015. Kwa nini hawakukemewa wote kwa pamoja?.Lakini pia Paul
Makonda amewakashifu viongozi wetu wa dini kwa kuwafanisha na wasaka pesa
kwahili tunamtaka awaombe viongozi hawa wote msamaha haraka,Vilevile ieleweka
viongozi wa dini ni nguzo ya vijana wa taifa hili na uvccm inawathamini na pia
tunatoa rai kwa mtanzania yoyote mwenye imani na roho ya upendo na wa dii
yoyote kufanya kazi na viongozi wa dini
na kujenga nchi pamoja nao,Je Mzee Malecela anaunga mkono Paulo Makonda
kuwakashifu viongozi hawa wa dini?.Tulitegemea sana Mzee kama Malecela
angekemea matendo haya kwa wanachama wote lakini ameonesha chuki binafsi kwa
ndugu Edward Lowassa. Lakini hatupaswi kumshangaa maana hata Hayati Mwl Nyerere
aliposema kama Mzee Malecela atagombea Urais narudisha kadi ya CCM,
Hatukumuelewa Mwl Nyerere alimaanisha nini lakini kwa sasa tumepata picha
kamili ni jinsi mzee huyu asivyo na busara na anaweza kukizamisha chama kwa
chuki zake binafsi na maneno yake ya kupotosha watanzania.
Mzee
Malecela anapaswa kuomba radhi kwa Umoja wa Vijana wa CCM kwa kumuunga mkono
Paul Makonda ambaye si msemaji wa UVCCM kwa mujibu wa Kanuni za Umoja wa
Vijana. Wasemaji wakuu wa Jumuiya ni Mwenyekiti na Katibu kwa ridhaa ya vikao
na maadhimio yaliyofanywa katika vikao wao ndo wenye mamlaka hayo. Lakini pia
Makamu mwenyekiti Mboni Mwita amekana kutolitambua tamko la Umoja wa Vijana
bali ni la kwake binafsi tunashangaa Mzee Malecela kwa nini anamuunga mkono
Paul Makonda.
Tunatoa
wito kwa Chama cha Mapinduzi kupiga marufuku matamko yote yanayoendelea nchini
na kuwachukulia hatua wale wote wanaotangaza nia ya kugombea Urais kabla ya
wakati na tunamuomba Mh. Mwenyekiti wa Chama ndugu Jakaya Mrisho Kikwete
kukemea hali hii kwa nguvu zake zote ili kukisalimisha Chama na kuwepo kwa utii
wa Kikatiba. Kuachwa kwa hali kama hii itakuza migogoro na makundi ndani ya
Chama.
Imetolewa
na Komredi Heri Hoza ni Kada wa muda mrefu wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati ya
Utekelezaji ya baraza la Umoja wa Vijana wa ccm Mkoa wa Morogoro. Pia ni
Mwenyekiti wa CCM wa tawi jipya la Chuo Kikuu huria (Morogoro branch).
2 comments:
Alikatazwa lowasa kushika madaraka yeyote katika nchi hii,
Wewe kwani Ni msemaji WA nani?
Lowasa kakuahidi nini?
Nini faida ya kumsemea?
Uchunguzwe something wrong !
2015............mkimteua imekula kwako na chama chako!
PIA na wewe unajichanganya kama uliona wamekosea huyo malecela SI waachie wahusika wewe ukasema kama nani at???/Na kulikuwa na mkutano WA kuazimia kuwasema??
Dar es salamaaaa alitengeneza mafulana kwa waendesha tukutuku zaidi ya 30,000 na kuwaahidi kila mtu atapata pikipiki,???????!!!!inashangaza Sana,Je mafuriko ya morogoro Kachangia nini????
Nyie lenu moja hueleweki kama kinyonga ki usalama WA chama chako inatakiwa uchunguzwe
Tafakuri m badala
Uvccm Moro mnajingusha kwenye penati box..acheni njaaa
Post a Comment