Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini na landcruiser VX iliyokuwa imewabeba wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyobwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni hii
Friday, 28 February 2014
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi. |
Wednesday, 26 February 2014
MBUNGE AOKOA MAISHA YA DEREVA TAXI ALIYEKUA ANATAKA KUWAWA NA WANANCHI BAADA YA KUMGONGA BODA BODA
Wananchi wa Tanangozi katika wilaya ya Iringa wakimsaidia kijana mwendesha boda boda asiye na viatu baada ya kugongwa na taxi yenye namba T 6338 AWV mbele |
Tuesday, 25 February 2014
UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA : CCM WAENDELEA NA KAMPENI
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu akimnadi mgombea ubunge kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Kalenga, Godfrey Mgimwa |
ANGALIA PICHA DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI
Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.
Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza
TAARIFA KAMILI SAKATA LA MADIWANI WA CHADEMA KUJIUZULU SHINYANGA
Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa viongozi ngazi ya taifa wa chama hicho kundekeza majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi pamoja na kuwapa majina ya wasaliti wa chama. |
MBUNGE ABOOD AMWAGA MISAADA KWA VIKUNDI VYA VIKOBA NA VIJANA MORO
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akitoa jezi kwa wachezaji wa timu ya maskani Fc iliopo kata ya Mjimpya mjini hapa.
Mbunge huyo akisalimia na diwani wa kata ya Mindu Hamis Msasa akiteta jambo na mbunge huyo nje ya ofisi ya mbunge huyo jana.
Mbunge wa jimbo la Morogoro Aziz Abood akitoa hundi kwa kikundi cha wanawake cha vikoba cha mjini hapa.
Viongozi wa kikundi cha vikoba cha wanawake polisi cha mjini hapa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea hundi shilingi 300,000 kwaajili ya kutunisha mfuko wao kutoka kwa mbunge wa Morogoro mjini.
mbunge huyo akitoa hundi kwa kikundi hicho cha wanawake polisi
kikundi cha wanawake cha kupika cha Mazimbu mjini hapa wakipokea vyombo vya kufanyika kazi kutoka kwa mbunge huyo
Habari zaidi soma hapa
MBUNGE wa jimbo l a Morogoro mjini Abdullazizi Abood ametoa msaada wa
fedha na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 2.53 kwa
vikundi vya wanawake nane vilivyopo katika manispaa ya Morogoro ikiwa ni
kuelekea siku ya wanawake duniani.
Akitoa hundi ya fedha kwa vikundi hivyo Abood aliwataka wanawake hao kuhakikisha wanatumia msaada huo wa fedha kwa manufaa ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Aidha Abood alisema kuwa kuwapo kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini kunalenta maendeleo ya dhati na hata wanawake kuthaminiwa na waume zao kutokana na kuongezeka kwa kipato katika familia zao.
“Misaada ninayotoa kwamba nina fedha sana ila najua majukumu waliyonayo wanawake nchini hasa katika jimbo langu kwani nimeweza kufanya ziara jimbo langu lote na kujionea matatizo ya wanawake yanayowakabili,na nia yangu ni kuhakikisha wanajikwamua na umaskini na kuweza kujitegemea wenyewe”alisema.
Mwenyekiti wa kikundi cha Polisi Slab vikoba Ukende Ugula akizungumza kwa niaba ya wenzake alimuomba mbunge huyo kuendelea kutetea haki za wanawake na ,watoto na kuhakikisha masuala ya wanawake yaliyopo katika rasimu ya katiba yanaingizwa katika katiba mpya.
Pia alisema kuwa bado kunatatizo la wanawake wengi hasa wa vijiji kutojua haki zao,na kumtaka mbunge huyo kutokata tamaa ya kusaidia wanawake hasa katika mkoa wa Morogoro.
Vikundi vilivyopatiwa msaada ni Tushikamane,Polisi Slab vikoba,Dirisha la maendeleo kutoka chuo cha maendeleo morogoro,Tujishike,Changamka,Ushindi,Tushikamane bigwa na kikundi cha mapishi cha Modeco kilichopatiwa vifaa vya kupikia na kugawa chakula.

Sunday, 23 February 2014
ANGALIA PICHA AJALI MBAYA YATOKEA MIKESE MOROGORO LEO ASUBUHI.
Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund
Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
ANGALIA PICHA MAUWAJI YA USTADHI NA MTOTO JAMALI SALUM L MBAGARA CHARAMBE
mwili wa maremu mtoto Jamali aliechinjwa na ustadhi mbagala charambe mianzini
mwili wa marehem ustadhi mohamed kurangwa aliemchnja mtotoukishushjwa katika hospitali ya Temeke |
Saturday, 22 February 2014
ROLI LAWAKA MOTO MORO
ROLI LIMEWAKA MORO KATIKA ENEO LA MIKESE WILAYA YA MOROGORO, KATIKA BARABARA YA MOROGORO NA DAR ES SALAAM. GARI HILO LIMEZIBA NJIA NA KUZUIA MAGARI MENGINE KUPITA. HABARI ZAIDI TUTAWALETEA HIVI PUNDE
ASKOFU MORO AOMBA SERIKALI KUWAONDOLEA KODI KATIKA VIFAA VYA HUDUMA ZA AFYA
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Mtakatifu Thomas kilichopo kata ya kilakala manispaa ya Morogoro.
Askofu wa jimbo katoriki la Morogoro Telesphori Mkude akizungumza katika hafla hiyo
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amazni naye alipata fulsa ya kuzungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa kata ya Kilakala akielezea jinsi walivyofarijika kupata kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bendera akiwa na viongozi wenzake katika picha ya pamoja.
Mkuu wa shirika la damu takatifu sista Claudia Maria akielezea historia ya kituo hicho.
Hii ni moja ya wodi ya wanaume katika kituo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizunguka kukagua mazingira ya kituo hicho
Wauguzi na wananchi wa eneo la jirani na kituo hicho wakifurahia katika uzinduzi huo.
Ulifika wakati wa kufungua muziki, viongozi hao waliondoka na miondoka ya mfano wa nyimbo za kabila la Kichaga wanaoshikana mikono .
Namie sikuwa mbali sanaa, hao wabibi nimekuwa nao tangu utoto wangu, tulikuwa tukisali pamoja katika kanisa la Kituo hicho, Tulikuwa wote katika Rejio Maria, nilifarijika sana nilipowaona nikaona niweke kumbukumbu.
Habari kamili soma hapa

ASKOFU wa jimbo Katoriki la Morogoro Teresphori Mkude
ameomba serikali kuwasaidia kuwaondolea kodi
kwa vifaa vya huduma za afya
wanavyoingiza ili waweze kuboresha zahanati na vituo vya afya katika
jimbo hilo.
Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha
St Thomas kilichopo kata ya Kilakala katika manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa wanafikiria zaidi kuboresha huduma ya afya
hususani vijijini na kwamba ili wafanikiwe
hakuna budi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kuwaondolea kodi hiyo.
Alisema kuwa tayari wameshaomba wafadhili kutoka nje
kwaajili ya kuwasaidia vitanda vitatu kwaajili ya kujifungulia wajawazito ili waweze kupeleka katika zahanati yao iliopo
Maskati Turiani wilayani Mvomero.
Pia aliomba serikali ya wilaya ya Mvomero kuwaboreshea
barabara ya kwenda Maskati ili iweze kufikika kwa nyakati zote na kuweza
kuwasaidia wagonjwa kufika katika zahanati hiyo kwa urahisi.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa
Serikali inafarijika kuona mashirika ya dini yanapotoa huduma hizo ambapo aliwahakikishia kuwa nao bega kwa bega
katika kufanikisha huduma hizo.
‘’ Tangu miaka ya zamani mashirika ya dini ndio yaliweza
kutoa huduma bora zaidi za afya na elimu, na tunatambua mchango wenu ndio maana
hata mnapohitaji watumishi hatusiti kuwapatia’’ Alisema
Naye mkuu wa shirika la damu takatifu linalomiliki Kituo
hicho cha Afya sista Claudia Maria alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka
1982 kama zahanati ambayo ilikuwa ikitoa huduma
kwa wagonjwa wa nje .
Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa huduma hiyo kwa
wananchi wa manispaa ya Morogoro waliamua kuboresha na kukipandisha hadi hadi
kufikia kituo cha afya .
Alisema kuwa kwa sasa
wanampango wa kujenga chumba cha upasuaji ili wajawazito wanaopatwa na
matatizo waweze kupata huduma hiyo hapo.
Alisema kuwa kituo hicho kinahudumia wagonjwa 1074 kati ya hao 289 ni
wa mfuko wa bima ya afya na kuongeza kuwa changamoto walionayo ni mfuko huo kuchelewesha
malipo na kusababisha upungufu wa dawa .
Friday, 21 February 2014
RAIS WA SHIRIKISHO LA RIADHA NCHINI MTAKA AMFAGILIA MEMBE KWA KUFADHILI WANARIADHA 40 MAFUNZO NJE YA NCHI
RAIS wa shirikisho la riadha Tanzania RT Antoni Mtaka amemshukuru waziri wa mambo ya nje Bernard
Membe kwa kufadhili wanariadha 40 kwenda nchi za China Uturuki na Kenya
kwaajili ya mafunzo.
Mtaka ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mvomero alisema hayo
Februari 21 mwaka huu wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema kuwa mafunzo hayo ni maandalizi ya mashindano ya
jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu nchini
Glassgon nchini Scotland.
Alisema kuwa wanariadha 20kati ya hao watakwenda nchini
China, wengine 10 watakuwa nchini
Uturuki, na 10 watakwenda nchini
Ethiopia sambamba na makocha 6 ambao nao
wanakwenda kupata uzoefu.
Alisema kuwa wanariadha 2 watakwenda nchini Kenya kwa ofa ya
waziri wa habari utamaduni na michezo Finela Mkangala ambaye alitoa ofa hiyo
wakati wa mbio za kifimbo cha malkia Elizabeth.
Alisema kuwa wanariadha wengine 35 watakuwepo hapa nchini
katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambao watachujwa na hao watakaotoka nje na
kwenda katika mashindano hayo ya jumuiya ya Madola.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuboresha mchezo huo na
kuweza kuleta ushindi hapa nchini badala ya kubakia kuwa kama washiriki au
watalii kama ilivyokuwa hapo awali.
‘’ Hatutaki kubakia kama watalii au washiriki sasa, tunataka
kuwa washindi, watakaokwenda ni wale tu wanaokidhi vigezo’’ Alisema
Pia Mtaka alitoa wito kwa wadau na viongozi mbalimbali kuiga
mfano huo kwa kuwasaidia wanariadha hapa nchini ili kukuza mchezo huo.
Alisema kuwa mbio hizo zitakazoshindaniwa ni pamoja na mbio
fupi, mbio za kati na mbio ndefu sambamba na marathon , miruko na mitupo.
Subscribe to:
Posts (Atom)